WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, amezindua rasmi Sherehe za Maadhimisho ya miaka 60 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD), sherehe ambazo zimefanyika viwanja vya Mahafali vilivyopo chuoni hapo.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Dkt. Gwajima aliimwagia sifa kem kem TICD kwa historia iliyotukuka katika utoaji wa elimu hapa nchini kwa kipinidi cha miaka 60 tangu kilipoanzishwa mwaka 1963.
‘’Kwa kweli, Miaka 60 ni kipindi kirefu. Ingekuwa ni umri wa binadamu, basi chuo hiki leo kingetambulishwa kama mzee mshauri mwenye busara katika jamii fulani. Hata hivyo, ni kweli kwa miaka 60 ya uhai wa Chuo hiki, ninathubutu kusema kuwa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru ni moja ya Taasisi kongwe za kujivunia katika kutoa wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii hapa Tanzania’’, alinukuliwa Dkt. Gwajima.
Aidha, alibainisha jinsi ambavyo awamu zote za uongozi wa nchi yetu (kuanzia awamu ya kwanza hadi awamu ya sita) zilivyoithamini kada ya Maendeleo ya Jamii hapa nchini Tanzania kutokana na umuhimu wa kada hiyo katika kuibua, kupanga, kuamua, kutekeleza, kusimamia, kufuatilia na kutathmini shughuli/miradi ya maendeleo ili kutatua changamoto za kijamii, kiuchumi, kimazingira, kiutamaduni na kisiasa.
Kwa namna ya pekee alimtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa jinsi anavyoithamini sekta ya Maendeleo ya Jamii hadi kupekekea kuanzisha rasmi Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Januari 22, 2022.
‘’Ni imani yangu kuwa wataalam wa maendeleo ya Jamii wataendelea kuenzi dhamira hiyo ya Mhe. Rais katika kuwezesha jamii kuwa na mtazamo chanya kuhusu maendeleo yao, kuondoa umaskini, maradhi na ujinga, kushughulikia changamoto za ukatili wa wanawake, watoto na wazee, kuwezesha wananchi kiuchumi, kuzingatia haki za wanawake na watoto, malezi na makuzi chanya ili kuwa na watanzania waadilifu, wazalendo na wanaofanya kazi kwa bidii’’ alisisitiza Dkt. Gwajima.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.