Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ameagiza kubomolewa kwa majengo yote yaliyojengwa kiholela katika maeneo ambayo yamepimwa na hayatakiwi kujengwa na kuzitaka mamlaka za Maji na Umeme Mkoani hapa kutopeleka huduma hizo katika maeneo hayo.
Dkt. Mahenge ameyasema hayo leo alipofanya ziara kukagua ujenzi holela unaofanywa na wananchi waliovamia na kujigawia maeneo katika hifadhi ya Milima Jijini Dodoma, na kushuhudia nyumba moja iliyojengwa katika eneo hilo iliyofikia katika hatua ya kuezeka licha ya kuwekwa kwa alama ya “BOMOA” tangu ikiwa katika hatua ya msingi.
“Ukishaona mtu amejenga msingi, swala la kumwandikia bomoa achana nalo, wewe ni kuufuta ule msingi yaani kuubomoa kabisa hayo ndio maelekezo yangu Mkuu wa Mkoa leo, haya yote mnayaendekeza, kwa sababu mkishamwandikia siku 30 anakuja anajenga zaidi na baadae inakuja huruma ya Mahakama kuwa mlikuwa wapi mpaka anajenga kufikia hatua ya kuezeka, kwa hiyo ukishajiridhisha kuwa eneo limepimwa na haliruhusiwi kujengwa iwe amejenga msingi, ukuta au jengo lolote bomoa” alimesisitiza Dkt. Mahenge.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema wao kama Halmashauri ya Jiji wamekua wakifanya kazi ya kudhibiti ujenzi holela lakini baadhi ya wananchi wamekua wakaidi, sheria ya Mipango Miji iko wazi kuwa hairuhusiwi kujenga katika maeneo ambayo yameachwa kama hifadhin ya milima.
Aidha, Kunambi amewataka wananchi kufuata sheria kwa kuwa haoni sababu ya watu kujenga kiholela katika maeneo ambayo hayajapimwa au yamepimwa lakini hayaruhusiwi kujengwa kwasababu Jiji la Dodoma bado lina viwanja vya kutosha ambavyo vimepimwa na vinaruhusiwa kujengwa makazi au Biashara.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (mwenye shati la bluu) akiwa katika ziara kuangalia maeneo yaliyovamiwa isivyo halali.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi (mbele) akiwa na Afisa Mdhibiti ujenzi holela Mhandishi Ally Bella walipotembelea maeneo yaliyofanyiwa uvamizi na kufanya ujenzi holela.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.