• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Dkt. Mahenge amuapisha Mafuru kuongoza Jiji la Dodoma

Imewekwa tarehe: August 21st, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge amempongeza Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo na akimtaka kufanya kazi kwa bidii na kudumisha ushirikiano baina ya Halmashauri hiyo na Ofisi ya Mkoa.

Dkt. Mahenge ameyasema hayo leo baada ya kuapishwa kwa Mkurugenzi mpya wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru tukio lililofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa. Mkurugenzi Mafuru anachukua nafasi ya Godwin Kunambi.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa Jiji la Dodoma liko kwenye makao makuu ya nchi na Kitovu cha shughuli za maendeleo ya nchi yetu, hivyo amemtaka Mkurugenzi huyo kuwa daraja la kuwaunganisha Wafanyakazi wa serikali kuu na serikali za mitaa huku akisisitiza kuwa mafanikio yanatokana na kuwa na umoja.

Aidha, amemtaka Mkurugenzi huyo kuendelea kutatua migogoro ya ardhi pamoja na kuzingatia sheria za Mipango Miji na kuendeleza Jiji kwa kufuata Mpango Kabambe wa Jiji ili kuyafanya makao makuu ya nchi kuwa na muonekano mzuri kwa sababu Dodoma ndio dira ya mikoa mingine nchini.

“Niwaombe watumishi wengine mpeni ushirikiano kijana mwenzenu kwasababu akifanikiwa yeye na ninyi mmefanikiwa kwa hiyo ili mfanikiwe ni lazima wote muwe na ajenda moja ya kuliendeleza Jiji la Dodoma” aliongeza Dkt. Mahenge.

Kwa upande wake Mkurugenzi, Joseph Mafuru amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua na kuona kuwa anafaa kuendana na kasi yake, huku akiahidi kufanya kazi kwa bidii na kudumisha ushirikiano ili kuleta maendeleo katika Jiji la Dodoma na Taifa kwa ujumla.

“Maendeleo haya yanayoonekana yametokea kwa viongozi waliotutangulia. Ninamshukuru sana Mkurugenzi aliyepita alitutengeneza tuje kuwa viongozi, na mimi naahidi nitafanya kazi na nitaendana na kazi ya Mheshimiwa Rais kama anavyotaka” aliongeza Mafuru.

Zoezi la kuapishwa Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma limehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Mkoa, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma na waandishi wa habari.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (kulia) akimpongeza Mkurugenzi mpya wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru mara baada ya kumuapisha kushika nafasi hiyo.



Matangazo

  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA USAHILI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA WASIMAMIZI JIMBO LA MTUMBA October 03, 2025
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA- DODOMA MJINI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA MAKARANI WAOGOZAJI WAPIGA KURA October 03, 2025
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Rc Senyamule awasihi wawekezaji sekta binafsi kuwekeza Dodoma

    October 03, 2025
  • CCTV kamera mwarobaini wa wavunjifu wa sheria jiji la Dodoma

    October 02, 2025
  • Wadau wa afya wapongezwa kwa juhudi zakudhibiti vifo vya wajawazito

    October 01, 2025
  • UONGOZI WA KLABU YA MICHEZO OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAKUTANA NA RAS KAZUNGU

    September 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.