MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kujengwa katika wilaya ya Dodoma na kuagiza hatua za haraka zichukuliwe ikiwemo kubomolewa majengo ya watu au kampuni zinazojenga bila kupata kibali cha ujenzi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Aidha, Dkt Mahenge amepongeza utaratibu wa wahandisi wa jiji kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika majengo mbalimbali yanayojengwa na kuwataka waandae taarifa ya miradi yote inayojengwa hapa jijini ili kuitambua mapema kabla ya kutembelea.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi ameahidi kusimamia zoezi la ukaguzi wa majengo mbalimbali yanayoendelea kujengwa na kuchukua hatua kwa watu wanaojenga bila vibali vya jiji. Aidha, amesema kuwa tayari jiji linatarajia kuongeza askari wake 20 ili kuimarisha oparesheni za ukaguzi.
"Jiji la Dodoma limeshika nafasi ya pili kwa kuwa na mtandao mrefu wa barabara za lami zinazofikia kilomita 130 likitanguliwa na Manispaa ya Kinondoni yenye mtandao wenye urefu wa kilomita 136".
Ziara hii ya siku mbili kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jiji la Dodoma inahuisha majengo ya watu binafsi, majengo ya serikali, miundombinu ya barabara, vituo vya afya, shule na usafi wa mazingira.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.