Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughurikia Afya Dkt. Charles Mahera amemuelekeza Mkurugenzi wa huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe kufuatilia na kuwachukulia hatua waratibu wa Mikoa ambao hawajawasilisha takwimu ya magonjwa wasiyoambukiza yakiwemo Sukari na Shinikizo la damu.
Dkt Mahera ametoa maelekezo hayo wakati akifungua kikao cha mwaka cha waratibu wa Mikoa wa magonjwa yasiyoambukiza Jijini Dodoma ambapo ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Singida, Kilimanjaro, Katavi, Rukwa, Tabora, Iringa, Mara, Dodoma na Mbeya.
“Hawa waratibu kama wameshindwa kazi wabadilishwe hatuwezi kuwa na waratibu ambao hawawezi kutupatia takwimu wanatukwamisha lakini tunawaita hapa tunawapatia posho na mnasikia haya magonjwa yanachangia asilimia 34 ya vifo hapa nchini na ili tuweze kupambana nayo lazima tuwe na takwimu” amesema
Katika hatua nyingine, Dkt. Mahera amewataka waratibu wa mikoa wa magonjwa wasiyoambikiza kuwa makini wakati wa kufanyia kazi changamoto na kuweka mikakati itakayotoa matokeo chanya katika kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza wakati wa kuandaa mpango kazi wa mwaka 2024/2025.
“Wataalamu tunayo fursa kubwa ya kuleta mabadiliko katika Afya ya jamii zetu kwa kujikita zaidi katika kuzuia na kudhibiti, napenda kusisitiza kuimalisha usimamizi katika ngazi ya Halmashauri na vituo” amesema Dkt. Mahera.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.