Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameridhishwa na utayari wa vyombo vya usalama kushiriki katika zoezi la upandaji miti nchini.
Dkt. Mpango alisema “shukrani kwa askari na makamanda. Moja ya sifa ya majeshi yetu ni nidhamu. Nataka kuona nidhamu hiyo iendelee kwenye upandaji na utunzaji wa mazingira. Jkt Makutopora wamefanya kazi nzuri sana. Napenda kuona hayo kwenye kambi zote”.
Vilevile, Makamu wa Rais alikipongeza chuo kikuu cha Dodoma kwa kuwa mfano mzuri katika upandaji miti na utunzaji wa mazingira. “Chuo kikuu cha Dodoma mmeonesha mfano wa kuwa wakereketwa wa mazingira. Wahimizeni wenzenu kujiunga na club ya mazingira” alisema Dkt. Mpango.
Kwa upande wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo alisema kuwa maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yanafanyika kitofauti. “Nawashukuru walimu na wanafunzi wanafanya vizuri katika utunzaji mazingira na upandaji. Chama cha Mapinduzi kupitia vijana wake wamekuwa wachagishaji wakubwa katika zoezi la unandaji miti. Vyuo vyetu vya Dodoma pia vinashiriki vizuri” alisema Dkt. Jafo.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alisema kuwa Mkoa wa Dodoma upo salama. “Mkoa wa Dodoma tutaendelea kusimamia yaelekezo yako uliyoyatoa kwetu na kusimamia mikakati ya kutunza mazingira. Aidha, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina jumla ya maeneo 162 ya wazi, maeneo 40 yamepata wadau wa kuyatunza na kuyaendeleza” alisema Senyamule.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.