• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Dkt. Mpango atoa pongezi maandalizi ya Nanenane

Imewekwa tarehe: August 1st, 2025

Na. Tutindaga Nkwindi, DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango atoa pongezi kwa maboresho katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi katika maonesho ya kitaifa ya Nanenane kwa kuongeza matumizi ya teknolojia ya kisasa.

Alitoa pongezi hizo wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya 32 ya wakulima Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Dkt. Mpango alieleza kuwa serikali imefanya maboresho makubwa yanayoonekana katika sekta hizo, ikiwemo kuimarisha uhifadhi wa mazao ya wakulima, utoaji wa chanjo kwa mifugo, na utambuzi wa mifugo kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Aidha, alisisitiza dhamira ya serikali kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha chakula barani Afrika kwa kuweka mkazo kwenye uzalishaji wa mazao ya kimkakati yenye thamani kubwa ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. “Viongozi wote katika ngazi mbalimbali wanapaswa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sera za kilimo na kuwahimiza wananchi kutumia ardhi kwa tija, hususani kulima mazao yanayostahimili ukame” alisisitiza Dkt. Mpango.

Alisema kuwa maonesho ya Nanenane ni kiashiria cha uwezo wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kuwa na upatikanaji wa chakula cha kutosha. “Ndugu wananchi, sekta ya kilimo imeendelea kufanya vizuri sana na inaashiria upatikanaji wa chakula ni toshelevu. Wataalam waendelee kutusaidia kutoa elimu ya kutosha na kufanya tafiti yakinifu katika kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi” alisema Dkt. Mpango.

Maonesho ya Nanenane hutoa fursa kwa wakulima, wafugaji, na wavuvi kutoka maeneo mbalimbali nchini kuonesha ubunifu, teknolojia, na mafanikio waliyopata katika sekta zao. Kaulimbiu ya mwaka huu ni “chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi, 2025.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Serikali yaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza- Mwambene

    August 18, 2025
  • Afisa elimu mkoa wa Dodoma akagua maandalizi ya Juma la elimu ya watu wazima

    August 17, 2025
  • Wafanyabiashara wa mkoa wa Dodoma watangaziwa fursa za biashara nchini indonesia

    August 16, 2025
  • Wafugaji waaswa kufuga kwa kuzingatia uwezo wa malisho ili kupata tija

    August 15, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.