Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde amewataka walimu kote nchini kubadili mtazamo na kuacha kufundisha kwa mazoea badala yake kumuwezesha mwanafunzi kuwa na uelewa.
Dkt. Msonde amesema hayo katika kikao kazi kati ya Walimu,Maofisa Elimu,Wakuu wa Shule,Walimu Wakuu,Wawakilishi kutoka Chama cha Walimu Tanzania,Ofisa kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu wa wilaya ya Sikonge kilichofanyika katika shule ya Sekondari Kamagi Tarafa ya Sikonge halmashauri ya wilaya ya Sikonge.
Dkt. Msonde amewambia walimu “Tuna kazi kubwa ya kufanya jambo la kuboresha elimu mkumbuke tuna vita na isewe mazoea ‘business as usual’ kwahiyo kila mmoja wenu akili yake izame kwamba serikali ya awamu ya sita imedhamilia kwa dhati elimu Tanzania iwe bora na anayeleta ubora wa elimu ni wewe(mwalimu) na lazima tufanye vitu tofauti na kuachana na mazoea kwasababu ni vita” amesema Dkt. Msonde
Dkt. Msonde ameongeza kuwa walimu wa shule za sekondari wahakikishe wanafunzi wanajua lugha ya kingereza kwa kusikia,kusoma na kuongea badala ya kukimbizana kumaliza mada(topics) na kuiacha idadi kubwa ya wanafunzi bila uelewa.
“Tulifundishwa chuoni kuwa furaha ya mwalimu ni pale ambapo mtoto anayemfundisha amemuwezesha kupata ujuzi na umahiri hatukufundishwa chuoni kuwa raha ya mwalimu ni kukata mada zote ziishe” amesema
Aidha,Dkt. Msonde amewataka walimu kuzingatia mambo manne wakati wa ufundishaji ambayo ni kujua uwezo wa mtoto,kujua utayari wa mtoto anayemfundisha,mazingira ya mwanafunzi na umri.
Kwa upande wake Ofisa Elimu mkoa wa Tabora Mwl. Juma Kaponta amesema atahakikisha anasirikiana na walimu kuhakikisha maelekezo yaliyotolewa wanafanyiwa kazi na kuleta matokeo chanya katika mkoa wa Tabora
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.