NDEGE mpya mbili aina ya Airbus A220-300, zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania zimewasili nchini kutokea Canada.
Ndege hizo zimepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume Mjini Unguja, Zanzibar leo Oktoba 8, 2021 majira ya saa 9:00 Alasiri na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Ndege hizi ambazo zimepewa majina ya Zanzibar na Tanzanite zinakamilisha hesabu ya ndege 11 zilizonunuliwa na kuwasili hapa nchini.
Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezungumza na Watanzania katika mapokezi hayo na hapa ni baadhi ya nukuu zake.
"Wanachi wa Zanzibar wana furaha kubwa kuona kwamba tukio hili la kihistoria la kupokea ndege hizi linalofanyika hapa Zanzibar".
"Bila shaka uamuzi wa kufanya mapokezi haya Zanzibar ni kielelezo cha juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na viongozi wa taifa hili katika kuendeleza na kulinda fikra, mawazo na falsafa za waasisi wa taifa letu katika kuulinda na kuudumisha Muungano wetu".
"Mapokezi ya ndege hizi mbili aina ya Airbus ni hatua muhimu katika juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania katika kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania ambalo lilianzishwa mwaka 1977".
"Sekta ya usafirishaji wa anga, majini na nchi kavu ni msingi muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa taifa letu".
"Nahimiza taasisi zetu zilizo katika viwanja vya ndege kufanya kazi kwa ushirikiano na ufanisi unaotakiwa".
"Naamini kwamba tukiwa na ndege zenye kufanya safari za moja kwa moja katika viwanja vyetu , sekta ya utalii na biashara zitaimarika kwa kasi".
Na hapa ni nukuu za Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa.
"Leo hii ni siku ya furaha kwetu watanzania kwa mapokezi ya ndege zetu mbili mpya, ikiwa zinakamilisha ndege 11 ambazo zimenunuliwa kwa fedha yetu watanzania".
"Ununuzi wa ndege hizi ni kwa ajili ya kuongeza safari za ndani, nje na safari hizi ni kwa ajili ya kuongeza fursa kujiongezea uchumi wa taifa au wa mtu mmoja mmoja kwa wale ambao wataamua kufanya biashara zao kupitia ndege hizi".
Aliyosema Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa
"Kuwasili kwa ndege izi mbili kutaifanya ATCL kuendelea kutoa huduma za uhakika, kuongeza miluko kwa safari za ndani,na kuweza kuanzisha safari mpya za kikanda katika miji mikuu ya biashara ikiwemo kinshasa,lubumbashi,Nairobi na Ndola".
Nukuu za Mkurugenzi mtendaji wa ATCL Injinia Ladislaus Matindi
"Ndege zedtu zimeletwa na marubani wetu wenyewe na waandisi na wote waliohusika katika makabidhiano na ukaguzi wa ndege wote ni watanzania tofauti na miaka iliyopita".
"Ndege hizi mbili zilizokuja leo ni toleo jipya ambalo tumeboresha baadhi ya vitu kutokana na mahitaji katika soko na zitatuweka katika hali nzuri ya ushindani".
"Ndege izi zina uwezo wq kubeba abiria 132 kila moja,ambapo abiria 12 wako katika daraja la biashara na abiria 120 katika daraja la uchumi na inaruka saa 6 bila kutua ikiwa na abiria na mizigo".
"Imewekewa mifumo ya kuwasaidia marubani kuruka na kutua ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi".
"Pia zimeongezwa kiasi cha kubeba uzito wakati wa kuruka kutoka tani 67.6 hadi tani 69.9".
"Ndege izi zimewekwa mifumo ya burudani zikijumuisha sinema za watoto,michezo ya watoto, vichekesho, miziki na mitandao ya internet (wi-fi)".
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kupokea na kuzindua ndege mpya mbili aina ya Airbus A220-300 kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja wa ATCL.
Chanzo: Idara ya Habari Maelezo
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.