Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaasa wataalam wa Sekta ya Afya kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
Ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagaua hali ya utayari wa kupambana dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona endapo utaingia Jijini Dodoma katika maeneo yote yaliyopangwa. "Elimu bado haitoshi, kila siku ni lazima tuhakikishe tunatoa elimu kwenye jamii ili watu waweze kuelewa, watu waelewe ugonjwa huu maana yake ni nini, na kwanini tunasisitiza watu wanawe mikono, kwanini tunasisitiza maji tiririka na sabuni" alimesema Dkt Ndugulile.
Ameongeza kuwa, ni muhimu kwa wataalam wa Sekta ya Afya kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi, huku akisisitiza kuwa si kweli kwamba matumizi ya vitakasa mikono (sanitizer) ni bora zaidi kuliko maji tiririka na sabuni. "Si kweli kwamba vitakasa mikono (sanitizer) ni bora zaidi kuliko kutumia maji tiririka na sabuni, tunahitaji tuwatoe hofu wananchi juu ya matumizi ya njia hizi mbili katika kujikinga dhidi ya ugonjwa huu" amekazia Dkt. Ndugulile.
Naibu Waziri huyo amesisitiza kuwa Wataaalam wa Sekta ya Afya kuongeza ubunifu katika kutoa elimu ili kuepuka upotoshaji unaofanywa na baadh ya watu katika jamii juu ya kutibu maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.
Aidha, Dkt. Ndugulile amewaagiza wataalam wa Sekta ya Afya kutumia njia nyepesi zaidi katika kutoa elimu ya ugonjwa wa Corona ili maambukizi haya yaweze kueleweka zaidi kwa wananchi.
Mbali na hayo, Dkt. Ndugulile amesema kuwa, Serikali inaendelea kuleta mahitaji ya vifaa vyote vinavyohitajika katika maeneo yaliyotengwa kwa wagonjwa wa maambukizi ya virusi vya Corona endapo watatokea Jijini Dodoma. "Niwahakikishieni vifaa vyote tutavileta, lakini pia niendelee kuwaomba tuwe imara muda wote, msisubiri ili kuweza kupamabana na ugonjwa huu nabidi kuwa mbelel muda wote" alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Miongoni mwa maeneo aliyotembelea ni Kituo cha Afya Mkonje, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya DCMS.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akinawa mikono kwa sabuni na maji tiririka kutekeleza jukumu la kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona alipotembelea Kituo cha Afya Mkonze Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Kituo cha Afya Mkonze kujionea jinsi Jiji la Dodoma lilivyojiandaa katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Mojawapo ya vyumba ambavyo vimeandaliwa maalum kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa watakaoathirika na maambukizi ya virusi vya Corona katika Kituo cha Afya Mkonze .
Jengo lililotengwa kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa wa Corona katika kituo cha Afya cha Mkonze Jijini Dodoma endapo atapatikana mgonjwa wa Covid-19.
Eneo lililotengwa kwaajili ya kuwatenga washukiwa wa ugonjwa wa Corona lililopo karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wataalam wa Sekta ya Afya wa mkoa wa Dodoma (hawapo pichani) katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma baada ya kutembelea vituo vya Afya na hospitali kuangalia maandalizi kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya Corona.
Baadhi ya watumishi wa Sekta ya Afya wakimsikiliza Naibu Waziri Dkt. Ndugulile (hayupo pichani)
Baadhi ya watumishi wa Sekta ya Afya mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Naibu Waziri Dkt. Ndugulile (hayupo pichani)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.