MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Joseph Mafuru amesema kuwa mradi wa Hoteli ya kisasa inayojengwa na Halmashauri hiyo unatarajiwa kukamilika mwezi ujao wa Aprili, 2021 na unatarajiwa kuwa chanzo kikubwa cha mapato endelevu ambapo kitaiingizia Halmashauri shilingi bilioni moja kila mwaka.
Mafuru amesema mradi huo utaenda sambamba na mradi mwingine uliopo Mtumba ndani ya Mji wa Serikali ukijulikana kama 'Government City Complex' ambao nao utakuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 800 kila mwaka.
Mafuru ameyasema hayo leo Machi 10, 2021 wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichokutana kujadili Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji hilo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi huyo alisema Dodoma City Hotel yenye ghorofa 11 itaanza kufanya kazi hivi karibu na itakuwa chanzo muhimu cha mapato kuanzia mwaka mpya wa Fedha na kwamba ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 9.99 ambazo zote zimetokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Katika kikao hicho, Baraza la Madiwani limepitisha bajeti ya shilingi 120,841,764,871 ambapo zinatokana na vyanzo vya ndani, Serikali Kuu, na Wahisani mbalimbali, ambapo zitatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo, utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii, pamoja na masuala ya utawala na uendeshaji wa Halmashauri.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.