Shirika la Reli Tanzania – TRC limesaini mkatabana kampuni ya CRRC International kutoka nchini China kwa ajili ya ununuzi waBehewa 1430 za mizigo zitakazotumika katika reli ya kisasa – SGR, hafla yautiaji saini imefanyika katika ukumbi wa mikutano makao makuu TRC Februari 08,2022.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikalina Shirika, ambapo Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Ujenzi naUchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TRC,Mkurugenzi Mkuu TRC, Wawakilishi wa kampuni ya CRRC International, Menejimentina Wafanyakazi wa TRC pamoja na wanahabari.
Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi naUchukuzi ameshuhudia zoezi la utiaji saini mara baada ya kupata taarifa fupi yamkataba wa ununuzi wa behewa hizo pamoja na maendeleo ya ujenzi wa reli yakisasa nchini kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosakuwa Ujenzi wa reli ya kisasa unaoendelea kwa sasa ni kipande cha Dar es Salaam– Morogoro umefika 95%, Morogoro – Makutupora umefika 81% na Mwanza – Isakaumefika 4%.
Hata hivyo Waziri Mbarawa alisema kuwa katikaBehewa hizo 1430 zitakazotengenezwa zipo Behewa 60 za mifugo ambapo Behewa mojaitakuwa na uwezo wa kubeba takribani Ngo’mbe 100 ambayo ni sawa na Ngo’mbe6,000 kwa behewa 60. Pia zipo behewa 50 maalumu kwa ajili ya kubeba magariambapo behewa moja itakuwa na uwezo wa kubeba magari madogo 8 ambayo ni sawa namagari 400 kwa behewa 50.
Mhe. Waziri alifafanua kuwa “kutokana na uwezomkubwa wa reli ya kisasa, behewa hizi zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguzamrundikano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam ambapo treni moja itakuwana uwezo wa kubeba Tani 10,000 kwa mkupuo ambayo ni sawa na malori 500” alisemaProf. Mbarawa.
Katika hatua nyingine, Mhe. Waziri aliwapongezawafanyakazi wa Shirika la Reli kwa usimamizi mzuri wa mradi wa ujenzi wa reliya kisasa na kuwaomba waendelee kuchapa kazi kwa kutumia weledi walionao najitihada ili kutimiza malengo ya Serikali ya kuhudumia wananchi na kukuzauchumi wa Taifa.
Mkurugenzi Mkuu TRC, Ndugu Masanja Kadogosakatika taarifa yake amesema kuwa,
“Mkataba huu ni wa ununuzi wa behewa 1430 za mizigo za reli ya kisasa ambaounagharimu Dola za Kimarekani Milioni 127.2, ni mkataba wa miezi 12 yaani mwakammoja utakaohusisha usanifu na utengenezaji wa behewa kwa ajili ya kubebamizigo ya aina mbalimbali kulingana na aina ya behewa na matakwa ya mteja kupitiareli ya kisasa”.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi mkuualiweka wazi kuwa aina ya behewa zitakazonunuliwa kupitia mkataba huu ni,behewa 600 aina CCB (Container Carrier Bogie) kwa ajili ya kubeba makasha,behewa 400 aina ya CLB (Covered Large Bogie) kwa ajili ya kubeba mizigo yajumla ikiwemo Sukari, Saruji, Chumvi, Pamba, Tumbaku na Kahawa, behewa 190 ainaya PTB (Petroleum Tank Bogie) kwa ajili ya kubeba mafuta aina zote, Behewa 70aina ya HLB (High Large Bogie) kwa ajili ya Mabomba, Mbao, Magogo na Vyuma,behewa 50 aina ya MGB (Motor Goods Bogie) kwa ajili ya kubeba magari na behewa50 aina ya CWB (Cattle Wagon Bogie) kwa ajili ya kubeba Ng’ombe.
Kwa upande wake Mwakilishi wa kampuni ya CRRCambaye ni Meneja Msaidizi Bw. Tang Yun Peng amesema kuwa “Leo ni siku nzurikwetu CRRC kwa sababu haikuwa rahisi kufikia hapa, nakumbuka mwaka janatulishiriki katika mradi wa uboreshaji wa reli ya kati, hivyo tuna ujasiri wakutosha kusanifu na kutengeneza behewa bora na imara kwa ajili yenu” alisemaBw. Peng.
Shirika la Reli Tanzania linatarajia kukamilikakwa manunuzi na kuwasili kwa behewa hayo mapema Februari 2023 ambako kutakwendasambamba na kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha piliMorogoro – Makutupora ambacho kwa umbali huo kutaweza kuleta tija na faidakatika uendeshaji wa huduma ya usafirishaji mizigo.
Chanzo: Tovuti ya TRC
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.