WAZAZI na walezi wa kata ya Chamwino Jiji la Dodoma, wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua yake ya kutoa fedha kupitia Halmashauri ya Jiji, kiasi cha milioni 59, kwa ajili ya ukarabati wa vyumba sita vya madarasa vinavyovuja na kusababisha wanafunzi na walimu kunyeshewa na mvua na kushindwa kusoma na kufundisha.
Shukrani hizo zilitolewa na wazazi na walezi hao mbele ya Naibu Meya wa Jiji la Dodoma Emmanuel Chibago,walipokuwa wakizungumza kwenye kikao cha mkutano wa hadhara wa kujadili maendeleo uliofanyika shule ya msingi Chamwino (A) Dodoma.
Asha Ramadhani, Mariam Hassani wakizungumza kwa niaba ya wazazi na walezi wezao kwenye kikao hicho cha maendeleo cha shule, walisema kuwa fedha zilizotolewa na serikali kwa kupitia Jiji la Dodoma,zitakuwa mkombozi kwa wanafunzi na walimu ambao kwa kipindi kirefu wananyeshewa wanapokuwa kwenye madarasa hayo ambayo mabati yeke ni machakavu.
“Tuna kila sababu ya kuishukuru Rais kwa kutoa kiasi hicho cha fedha cha milioni 59 kwa ajili ya ukarabati wa majengo hayo ya shule,hivyo ni imani yetu sisi kama wazazi wanafunzi wetu na walimu wetu, watakuwa sehemu salama na hata ufaulu sasa utaongezeka zaidi”Maliam alisema.
Awali akizungumza kwenye mkutano huo wa wazazi na walezi Diwani wa kata ya Chamwino Jiji la Dodoma,Jumanne Ngede,alisema kuwa kwa muda mrefu vyumba hivyo vya madarasa yapatayo sita ni machakavu na yanavuja ,kwa maana hiyo kupatikana kwa fedha hizo kero hiyo inaenda kutatuliwa .
“Ni imani yangu sasa wanafunzi watasoma mahali salama, walimu watafundisha kwa uhuru, na ufaulu utaongezeka zaidi,hivyo niwaombea wale wote watakaohusika na ukarabati fedha zitumike kwa malengo yaliyokusudia ukizingatia kuwa Rais Samia ameipa heshima Halmashauri kutupatia fedha hizo” alisema.
Hivyo wazazi na walezi mnatakiwa kuiunga mkono serikali chaini ya Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi kubwa zinazowekezwa kwenye elimu,kwa maana hiyo ninawaomba mshiriki katika kujitoa kuhakikisha ukarabati wa majengo hayo unafanyika kwa haraka na kwa uaminifu mno.
Diwani huyo amewataka wazazi kuhakikisha wanachangia kwa nguvu kazi pindi kwenye ukarabati huo utakapowadia ili wanafunzi na walimu waweze kuondokana na hadha inayowapata kwa kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha ili kuiunga serikali ambayo imetoa fedha hizo kupitia halmashauri ya Jiji.
Kwa upande wake Naibu Meya ya Jiji la Dodoma Emmanuel Chibago akizungumza na wazazi na walezi wa kata hiyo ya Chamwino (A) ameiagiza kata na uongozi wake, kuhakikisha ukarabati huo unaanza mara moja ili kulitatua suala hilo lililopo kwenye shule hiyo ambayo majengo yake yanavuja .
Chibago alisema kuwa serikali kupitia Halmashauri ya Jiji bado itaendelea kuisaidia shule hiyo kwa kushirikiana na wazazi na walezi katika kutatua kero,hivyo niwataka kujitokeza kwa wingi kushiriki ili wanafunzi na walimu wawe salama kwenye maeneo husika.
Alisema kuwa shule ya msingi ya Chamwino serikali kupitia halmashauri inatambua kuwa ina mapungufu mengi,ikiwemo vyoo na madawati,hivyo hatuwezi kufuta siro wakati inakabiliwa na changamoto hizo hivyo ni lazima wazazi na walezi washirikiane katika kutatua kero hizo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.