TIMU ya Dodoma Jiji FC inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji inatarajia kusafiri leo Alhmisi Disemba 17, 2020 kuelekea Jijini Arusha kuikabili Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu ya VodacomTanzania Bara unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi hii.
Yanga ambao wanaongoza msimamo wa ligi hiyo ndiyo wenyeji wa mchezo huo ambao wameamua kuucheza kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta Jijini Arusha.
Msemaji wa Dodoma Jiji FC Ramadhani Juma alisema timu hiyo inatarajia kuondoka Jijini Dodoma majira ya mchana kuelekea Arusha kupitia Babati na kwamba uongozi umeshakamilisha kila kitu kuhusiana na safari hiyo.
Kwa upande wake, kocha mkuu wa timu hiyo Mbwana Makata alisema kuwa kikosi chake kina ari kubwa na kuahidi kupambana kufa au kupona kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa mgumu na kusisimua.
Dodoma Jiji FC inaelekea Arusha ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 ilioupata dhidi ya Gwambina ya Misungwi Mwanza kwa bao la Seif Karihe dakika ya 45 na kwa sasa timu hiyo ipo kwenye nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania Bara yenye timu 18.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.