Timu ya Dodoma Jiji FC kinara wa ligi daraja la kwanza imeendelea kujinoa na mazoezi makali kuelekea kukabiliana na hasimu wake Ihefu SC ambayo ipo nyuma kwa alama tatu akishikiria nafasi ya pili.
Kwa mujibu wa maelezo ya Kocha wa Dodoma Jiji FC, Mbwana Makata amesema kikosi chake kinaendelea na mazoezi ilikuwa imara zaidi kuelekea kumkabili mpinzani anayewafuatia kwani kila mechi sasa ni fainali katika mzunguko wa pili wakati wakiongoza ligi daraja la kwanza.
Mbwana ameendelea kusisitiza hamasa kutoka kwa mashabiki, waendelee kuipa 'sapoti' timu yao ili iweze kuendelea kufanya vizuri. Kwenye mzunguko wa kwanza Dodoma Jiji FC ilipata ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Ihefu SC uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
“Dodoma Jiji FC katika msimamo wa ligi kwa sasa tuko katika nafasi nzuri, hata hivyo hatujalidhika bado, tunaendelea kupambana ili tujiweke katika nafasi nzuri zaidi ya kupanda ligi. Kila mechi kwetu tunaicheza kama fainali, kumbuka tumecheza mechi tatu mfululizo hatujafungwa.
Tumejiandaa vizuri mechi inayokuja na Ihefu kwa sababu tumewazidi alama tatu, kila timu inang’ang’ana kuwa kileleni, cha msingi tunaujua ugumu wa mechi, ndiyo maana tunajinoa na mazoezi tuone makosa yaliyopita na kuyarekebisha ili tutengeneze 'game plan' kwa ajili ya mechi ijayo,” alisema Makata.
Kwa upande wake msemaji wa timu ya Dodoma Jiji FC, Ramadhani Juma ametoa wito kwa mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi ili kutoa hamasa kwa vijana hao wazidi kufanya vizuri zaidi na zaidi.
“Timu yetu inajituma na ipo chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Jiji, nitoe wito kwa makampuni binafsi au kwa yeyote kwa ajili ya udhamini dirisha liko wazi, pia kwa yeyote anahitaji kuichangia timu kwa hali na mali anakaribishwa ili tuweze kuisongesha mbele timu yetu.
“Kikubwa tu mashabiki wetu nawapongeza sana kwa kuendelea kuwa bega kwa bega na sisi na niwaombe tuendelee 'kuisapoti' timu yetu. Nina imani hata Mbeya tutakuwa wote, niwaahidi tu hatutawaangusha kwani Dodoma Jiji FC iko kwa ajili ya kuwafurahisha na kufika juu kileleni” alisema Juma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.