BAADA ya kupoteza mchezo kwa tabu dhidi ya Yanga Jumamosi iliyopita, timu ya Dodoma Jiji FC iliyo chini ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma inatarajia kujitupa dimbani kesho Jumatano Disemba 23, 2020 kwenye uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro kuivaa Mtibwa Sugar ya huko.
Mchezo huko unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwani unakutanisha timu zenye wachezaji wazuri.
Msemaji wa Dodoma Jiji Ramadhani Juma alisema timu hiyo tayari ipo Mkoani Morogoro tayari kwa mchezo huo utakaopigwa saa 10:00 jioni na kurushwa moja kwa moja na kituo cha matangazo ya televisheni cha Azam.
Juma alitoa wito kwa mashabiki na wadau wote kuendelea kuiunga mkono timu yao bila kujali inashinda au inapoteza mchezo kwani kwenye soka kuna matokeo matatu ya kushinda, kufungwa, au kutoka sare hivyo kila mdau wa timu hiyo anapaswa kulikubali jambo hilo.
Kocha Mkuu wa kikosi hicho Mbwana Makata alisema wamejiandaa vizuri kuikabili Mtibwa ugenini na kwamba anaamini watapata matokeo chanya na kuendelea kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.