Timu ya Soka inayomilikiwa na Jiji la Dodoma, Dodoma Jiji FC imeanza mazoezi ya kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza tarehe 6/9/2020.
Akizungumza na Mwandishi wetu, Afisa Habari wa Timu hiyo Ramadhani Juma (Raju Boy) amesema kuwa timu iliingia kambini mwishoni mwa wiki iliyopita na leo imeanza mazoezi rasmi chini ya Mwalimu Mbwana Makata.
“Kama mnavyojua tulikua mapumzikoni lakini pia tulikua na zoezi la usajili ambalo linaendelea, sasa baada ya asilimia kubwa ya wachezaji wapya na wale walioongezewa mikataba kuwasili kambini uongozi uliazimia kuwa leo mazoezi yaanze na tunashukuru hilo limewezekana mazoezi yameanza rasmi” Alisema Juma.
Aidha Juma amesema kuwa wachezaji wote wamewasili kambini isipokua wanne ambao watawasili kesho siku ya Jumanne, huku akiongeza kuwa bado zoezi la usajili linaendelea na zimebaki nafasi mbili za beki wa kulia na Kiungo mshambuliaji ambazo zitajazwa hivi karibuni kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.