Timu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, Dodoma Jiji FC imeendelea na mazoezi kujiandaa na mzunguko wa 19 wa Ligi hiyo.
Akizungumza na mwandishi wetu Kocha Mkuu wa timu hiyo Mbwana Makata amesema kuwa hali yakikosi chake iko vizuri na wameanza mazoezi ya nguvu kujiandaa na michezo mitatu ya nyumbani huku akiwahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuchukua pointi zote tisa katika dimba la Jamhuri Jijini hapa.
Makata amesema kuwa lengo la timu hiyo kwa msimu huu ni kubakia katika ligi hiyo kwa kumaliza wakiwa nafasi muhimu za juu.
“Kila timu inamalengo yake ambayo hujiwekea na hupambana ili kuyafikia au kuyavuka na sisi kama Dodoma Jiji FC tumejiwekea malengo yetu ambayo tunaamini tutayafikia na hata kuyavuka ikiwa ni pamoja na kusalia katika ligi huku tukimaliza katika nafasi za juu ili kuwapa furaha mashabiki wetu” Alisema Makata.
Akizungumzia kuhusu wachezaji wanaoweza kuikosa michezo hiyo Makata amesema kuwa kikosi chake kina majeruhi mmoja Rajab Mgalula ambae ameanza mazoezi mepesi, lakini pia Anuary Jabir na Anderson Solomon ambao wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 20.
Timu ya Dodoma Jiji FC itashuka dimbani siku ya Jumapili tarehe 14/02/2021 saa 10:00 jioni kuikabili JKT Tanzania katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.