Na. Asteria Frank, DODOMA
Dodoma Jiji Fc imejipanga vyema kwa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara utakao chezwa kesho saa 1:00 usiku dhidi ya Tabora United mzunguko wa saba mchezo wa 50 katika uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa NBC Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji Football Club Mecky Maxime alisema kuwa maandalizi yamekamilika kwa kuwa tumetoka kucheza mchezo mgumu dhidi ya Simba Sports Club juzi.
“Jana tumefanya mazoezi mepesi ya kuweka mwili timamu na baadhi ya majeruhi waliopatikana katika mchezo uliopita wanaenendelea na matibabu hivyo leo tutapumzilka ili wachezaji waingie na nguvu kwenye mchezo wetu ujao kama tuliyo tumia mchezo uliyopita” alisema Maxime.
Aidha, Nahodha wa timu ya Dodoma Jiji football Club Augustino Nsata alisema kuwa wapo tayari kupambania alama tatu katika mchezo wa kesho dhidi ya Tabora United licha ya wachezaji wenzie kutambua kuwa utakuwa mchezo mgumu na wala sio mrahisi ila wapo tayari kwa mchezo huo.
Alisema kuwa sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri kuelekea mechi ya kesho na tunaelewa ni mchezo mgumu sana kwetu, “wachezaji wote morari ipo juu kwasabau sisi kwetu kila mchezo ni fainali na ukizingatia katika mchezo wa kesho tupo nyumbani kwahiyo morari ipo juu na kila mtu anaelewa nini anatakiwa kufanya ili tuweze kupata alama tatu kwasababu tupo nyumbani na tunatamani kwamba hata mechi ingekuwa inachezwa leo” alisema Nsata.
Dodoma jiji inashikilia nafasi ya kumi kati ya timu 16 ikiwa na alama sita katika michezo wa sita ya ligi kuu Tanzania bara.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.