TIMU ya Dodoma Jiji FC leo imepoteza mchezo wake dhidi ya maafande wa Polisi Tanzania kwa mabao 3 - 0 katika mchezo mkali uliochezwa kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi.
Kwa matokeo hayo Dodoma Jiji imeshuka kutoka nafasi ya nne hadi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom 2020/21. Mchezo wa leo ambao ni wa raundi ya nne ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kupambana kupata pointi tatu muhimu.
Polisi walianza kujipatia bao la kwanza lililofungwa na Marcel Kaheza dakika ya 11 kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja na kumpita golikipa Aron Kalambo wa Dodoma Jiji.
Mpaka dakika 45 za mwanzo zinakamilika, Dodoma Jiji FC ilikuwa nyuma kwa bao hilo 1-0. Kipindi cha pili Polisi Tanzania waliongeza mabao mawili kupitia kwa Tariq Seif aliyefunga goli dakika ya 38 na goli la tatu likafungwa na Marcel Kaheza tena katika dakika ya 61 ya mchezo.
Akiongelea matokeo hayo mmoja wa viongozi wa timu Alfred Mlowe amesema wapenzi na mashabiki wa Dodoma Jiji wasikate tamaa kwa kuwa hiyo ndio hali ya mchezo. Ila wanarudi nyumbani kujipanga kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo inayofuata na watu waendelee kuipa 'support' timu yao.
Aidha, taarifa iliyotufikia imeeleza kuwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeufungia uwanja wa Ushirika Moshi kutotumiwa kwa michezo yoyote ya mashindano kutokana na kukosa baadhi ya sifa za kikanuni za sheria ya uwanja.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.