Uongozi wa timu ya soka ya Dodoma Jiji FC imeanza rasmi mbio za usajili kwa kuwasajili wachezaji watatu kutokea katika vilabu tofauti vya soka Tanzania bara.
Hayo yamebainishwa na Afisa Habari wa timu hiyo Ramadhani Juma kwenye taarifa yake kwa vyombo vya Habari ambayo imeorodhesha majina ya wachezaji walioachwa, walio ongezewa mikataba na wageni kutoka vilabu vingine nchini.
Juma amesema kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ni Cleophace Mkandala kutokea Tanzania Prisons ambaye pia anachezea timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa stars), Michael Chinedu kutoka Alliance pamoja na Seif Karie kutokea Lipuli wote wakisajiliwa kama wachezaji huru.
Akizungumzia wachezaji walioachwa Juma amesema ni Pamoja na Yusuf Abdul, Joseph Mapembe, Hamadi Kibopile, Rajabu Kibera, Joshua Soka, Aziz Gillah, Shabani Mocka, James Mendy, Ismail Makorosa, Moshi Mrisho, Mohamed Kilua na Ramadhani Mohamed ambaye amerejeshwa Azam FC baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika.
Vilevile, amewataja wachezaji walioongezewa mikataba kuwa ni Emmanuel Mseja, Hussein Masalanga, Anderson Solomon, Hassan Kapona, Mbwana Kibacha, Rajabu Seif, Steven Mganga, Jamal Mtegeta,Deusdelius Kigawa, Santos Thomas, na Khamis Mcha.
Aidha Juma amesema kuwa zoezi la usajili bado linaendelea na uongozi utaendelea kutoa taharifa Zaidi kuhusuana na usajili ndani ya miamba hiyo ya soka Jijini Dodoma.
Kiungo Cleophas Mkandala aliyekuwa timu ya Tanzania Prisons ya Mbeya amemwaga wino kuichezea timu ya Dodoma Jiji FC kwa mkataba wa miaka miwili. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji FC Fortunatus Johnson wakati wa utiaji saini katika ofisi za Jiji la Dodoma.
Golikipa wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) aliyechezo machindano ya AFCON Aaron Kalambo aliyekuwa Mbeya City FC rasmi amesajiriwa na timu ya Dodoma Jiji FC. Pembeni kushoto ni Dickson Kimaro na kulia ni Ally Kheri Mohamed ambao ni viongozi wa Dodoma Jiji.
Mshambuliaji mahiri Michael Chinedu aliyekuwa Allience ya Mwanza akikamilisha taratibu za kujiunga na timu ya Dodoma Jiji FC jijini Dodoma leo.
Seif Karie mshambuliaji aliyekuwa akikipiga katika timu ya Lipuli FC ya Iringa sasa rasmi ametua Dodoma Jiji FC tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom 2020/2021.
Mfungaji bora namba 2 wa Ligi Kuu ya Tanzania bara msimu wa 2019/2020 Peter Mapunda ametua rasmi Dodoma Jiji FC akitokea Mbeya City FC kwa mkataba wa miaka miwili. Kushoto ni Afisa Habari wa Dodoma Jiji FC Ramadhani Juma na kulia ni kiongozi wa Ally Kheri Mohamed wakishuhudia.
Kiongozi wa Dodoma Jiji FC Fredrick Mwakisambwe akibadilishana nakala ya mkataba na mchezaji mpya wa Dodoma Jiji FC Aaron Kalambo aliyekuwa Mbeya City FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.