TIMU ya Soka ya Dodoma Jiji Football Club mapema leo tarehe 27 Septemba 2021 imetangaza na kutambulisha rasmi jezi zake mpya kutoka kwa udhamini mnono wa miaka mitatu wa kampuni ya 10BET inayojihusisha na michezo ya kubashiri matokeo ya michezo barani Afrika.
Akizungumza katika tukio hilo maalum, Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabiri Shekimweli alipongeza wadau na viongozi wa Jiji hilo kwa kushikamana bega kwa bega na klabu huku akiwataka kuhakikisha kwa sasa wanatimiza lengo la kushika nafasi za juu mwisho wa msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (TPL 2021/2022).
"Tujipongeze kwa pamoja mafanikio ya timu yetu. Kwa udhamini huu wa zaidi ya Bilioni Moja uwe chachu ya kushika nafasi za juu mwisho wa msimu." Alisema Mkuu wa Wilaya Mhe. Shekimweli.
Shekimweli amewataka Madiwani wa Jiji la Dodoma kuhamasisha kila mechi waweze kujitokeza kwa wingi ilikuleta hamasa na timu ifanye vizuri kupata matokeo ya ushindi.
"Michezo ni ajira. Dodoma Jiji FC inauwekezaji wa fedha zaidi ya Tsh. Bilioni moja... Uwekezaji mkubwa sana huu. Nataka uwekezaji huu uendane na matokeo uwanjani."
Pia huongeza ajira kwa vijana kupitia michezo. Timu yetu kwa sasa iwe ya mfano na Waheshimiwa Madiwani kila mechi muhamasishe wananchi na waujaze uwanja nusu wao nusu sisi." Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma, Mhe. Anthony Mavunde ambaye ni mlezi wa timu hiyo amewashukuru viongozi wa timu na wadau wakiwemo mashabiki kwa ushirikiano mzuri na timu hiyo changa kuwa ya mfano.
"Dodoma Jiji Fc licha ya kuwa changa lakini imefanya vizuri sana na inamipango mikubwa.
Kuanzia sasa uwanja wa Jamhuri hatoki mtu. Niwaombe sana tujitokeze kwa wingi kuishangilia timu yetu kuanzia kesho tutakapoanza kucheza" Alisema Mhe. Mavunde.
Kwa upande wake, Katibu wa timu hiyo ya Dodoma Jiji FC, Fortunatus Johnson alisema udhamini huo umewaongezea hali ya kufanya vizuri kwenye mechi zao ikiwemo inayotarajiwa kuanza kesho dhidi ya Ruvu Shooting katika uwanja aa Jamhuri.
"Uongozi wa Dodoma Jiji FC umefurahishwa na kuvutiwa na mkataba huu ambao utakuwa chachu kwa klabu yetu.
Utasaidia klabu yetu kuleta ushindani mkubwa kwenye medani za soka na kuwapa fursa kubwa wachezaji wa timu yetu kuongeza ufanisi katika msimu huu wa 2021/2022 unaotarajiwa kuanza leo." Alisema Fotunatus Jonson
Aidha, amebainidha kuwa, udhamini huo wa 10BET kwa msimu wa kwanza wanagharamia vifaa mbalimbali vya wachezaji vitakavyotumika kwenye mazoezi na mechi.
"Mtengenezaji wa vifaa ni kampuni ya MASITA. ni jezi nzuri na zenye ubora wa hali ya juu.
Tuna jezi aina nne ikiwemo ya nyumbani, jezi ya ugenini na jezi zingine ambazo ni za kipekee" Alisema.
Kampuni ya 10BET inajishugulisha na ubashiri ya michezo na Casino ambayo inaendesha shughuli zake katika nchi 12 mpaka sasa hapa Barani Afrika huku ikiwa na uzoefu wa miaka 16 wakiwa na maono kuwa kampuni kinara, ya kuvutia na inayopiga hatua katika ubashiri wa matokeo ya michezo.
Timu ya Dodoma Jiji FC imekuwa na bahati ya kipekee kwani kwa Bara la Afrika imeweza kupata udhamini huo wa 10BET huku ikijiweka katika mstari wa mbele kwenye michezo kwa kugusa matukio makubwa ikiwemo Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, NBA na ile ya kuchezeshwa na kompyuta (Virtual Sports).
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweli akiongea wakati wa uzinduzi wa jezi na utambulisho wa mdhamini wa Dodoma Jiji FC ambaye ni kampuni ya 10BET.
Baadhi wa Waheshimiwa Madiwani wa Jiji la Dodoma wakifuatilia uzinduzi wa jezi na utambulisho wa mdhamini wa Dodoma Jiji FC, timu hii imepata udhamini kutoka kampuni ya 10BET.
Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Emmanuel Chibago (katikati) katika picha wakati wa uzinduzi wa jezi na utambulisho wa mdhamini wa Dodoma Jiji FC.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mhe. Anthony Mavunde (katikati) ambaye pia ni mlezi wa Dodoma Jiji FC wakati wa uzinduzi wa jezi na utambulisho wa mdhamini wa timu.
Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira wa Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro (katikati) ambaye pia ni miongozi wa viongozi wa Dodoma Jiji FC wakati wa uzinduzi wa jezi na utambulisho wa mdhamini wa timu.
Mchumi wa Jiji la Dodoma, Francis Kaunda (katikati) ambaye pia ni kiongozi wa Dodoma Jiji FC wakati wa uzinduzi wa jezi na utambulisho wa mdhamini wa timu.
Viongozi kutoka taasisi mbalimbali Jijini Dodoma (waliosimama) ambao nao walishiriki kwenye uzinduzi wa jezi na utambulisho wa mdhamini wa timu ya Dodoma Jiji FC.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma (waliosimama) walioshiriki uzinduzi wa jezi na utambulisho wa mdhamini wa timu inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma..
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweli alipokuwa akiongea na wadau wa timu ya Dodoma Jiji FC wakati wa uzinduzi wa jezi na utambulisho wa mdhamini wa timu.
Katibu wa timu ya Dodoma Jiji FC, Fortunatus Johnson.
Msemaji wa Timu ya Dodoma Jiji FC Moses Mpunga wakati wa uzinduzi wa jezi na utambulisho wa mdhamini wa timu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.