• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Dodoma Jiji U-20 yakita Kambi Kileleni

Imewekwa tarehe: January 23rd, 2025

Na. Mussa Richard, DODOMA

Klabu ya soka ya Dodoma Jiji chini ya umri wa miaka 20 (U-20) imeendeleza ubabe kwa wapinzani wake wanaoshiriki ligi ya vijana ya NBC chini ya umri wa miaka 20 Tanzania bara baada ya kuwashushia kichapo cha mabao 2-1 wanajeshi wa mpakani Mashujaa FC U-20, katika mchezo uliovulumishwa katika nyasi za dimba la Jamhuri Dodoma hapo jana.

Baada ya mchezo kutamatika kocha wa Dodoma Jiji U-20, Jeremiah Chido alisema “mchezo umemalizika salama na tumepata kitu ambacho tulikua tunakihitaji ambacho ni alama tatu muhimu. Alama ambazo zinatufanya tuendelee kuwa kileleni katika kundi letu na kutufanya tusicheze kwa presha michezo inayokuja mbele yetu, michezo ambayo tutakuwa ugenini”.

Katika hatua nyingine Chido akaweka wazi malengo yao kwenye msimu huu wa Ligi ya Vijana ya NBC Tanzania Bara. “Malengo yetu msimu huu ni kuchukua ubingwa kwasababu msimu uliopita tulifika fainali ila bahati haikuwa upande wetu. Kwahiyo, msimu huu tukishirikiana halmashauli, mashabikii, wachezaji na makocha mbalimbali hapa Dodoma nina uhakika tutachukua ubingwa wa Ligi hii ya vijana kwasababu rasilimali muhimu kwenye mpira ambayo ni wachezaji tunao na wanaonesha kila nia ya kuhitaji ubingwa” alisema Chido.

Kwa upande wake mchezaji wa Dodoma Jiji U-20, Christopher Shija ambaye ndiye kinara wa upachikaji mabao mpaka sasa katika ligi hiyo akiwa na mabao matano baada ya kumalizika kwa mchezo huo alisema malengo yake ni kuhakikisha anatwaa tuzo ya mfungaji bora wa ligi hiyo.

“Namshukuru Mungu mpaka sasa naongoza katika orodha ya wafungaji na sijaridhika bado nitaendelea kutumia nafasi kila nikizipata ili niweze kuwa mfungaji bora. Lakini pia niwashukuru sana wachezaji wenzangu kwasababu bila wao kunitengenezea nafasi nisingekuwa nafunga. Kwahiyo, tukiendelea kuwa na ushirikiano ndani na nje ya uwanja tutafanikiwa katika malengo yetu kama timu na mchezaji mmoja mmoja” alisema Shija.

Baada ya ushindi huo Dodoma Jiji U-20 imefanikiwa kukusanya alama 22 kibindoni ikishuka dimbani katika michezo tisa ikibakisha michezo mitano kumaliza hatua ya makundi, huku ikiendelea kushika usukani katika kundi A. Katika michezo iliyosalia Dodoma Jiji U-20 inahitaji walau alama mbili ili kujihakikishia kufuzu hatua ya robo fainali ya ligi hiyo ambayo inachezwa katika mfumo wa makundi mawili ambapo nafasi ya kwanza hadi ya nne kwa kila kundi moja kwa moja zinatinga katika hatua ya robo fainali.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.