NA THERESIA FRANCIS, DODOMA
Mratibu wa Sensa ya watu na makazi wa Wilaya ya Dodoma, Calister Makacha amewaasa Wakazi wa Wilaya hiyo kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa kujitokeza kuhesabiwa tarehe 23/08/2022 kwa maendeleo ya taifa.
Kauli hiyo aliitoa wakati akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
“Sensa ni zoezi zima la kukusanya taarifa, kuzichakata, kuzichambua na kutoa ripoti maalumu kwa ajili ya kukusanya takwimu za kidemografia, kiuchumi, mazingira lakini takwimu zote za watu pamoja na makazi yao” alisema Makacha.
Aidha, alielezea umuhimu wa zoezi hili kwa Serikali ya Tanzania kuwa zoezi hilo litasaidia kupata takwimu rasmi ambazo zitaisaidia katika kupanga mipango ya maendeleo ya taifa.
Sambamba na hilo, Machaka alielezea utaratibu wa Sensa hiyo ya sita toka zoezi la Sensa lianze mwaka 1967, kisha 1978, 1988, 2002, 2012 na sasa itakayofanyika mwezi Agosti 2022. Sensa hiyo itafanyika kwa njia ya kielektroniki kwa kutumia vishikwambi. Hivyo, makarani watakaoendesha zoezi hilo hawatakuwa na madodoso ya makaratasi kama ilivyokua miaka ya nyuma.
“Maswali yote yataingizwa kwenye vishikwambi na watahoji kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa dodoso kuu, dodoso la majengo na dodoso la makazi” aliongeza Makacha.
Sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022 inaongozwa na kaulimbiu isemayo “Sensa kwa maendeleo, jiandae kuhesabiwa”.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.