TIMU ya Dodoma Jiji FC (DJFC) imeyaanza vema mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuiadhibu timu ya Hollywood FC kwa mabao 5-1 kwenye mchezo uliochezwa leo, Januari 6, kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, na uongozi wa DJFC umeomba radhi kwa ushindi huo.
Ushindi huo umeiwezesha Dodoma Jiji kutinga hatua ya 32 bora ya Kombe la Azam Sports Federation linaloshikiliwa na Simba.
Mabao ya DJFC yaliwekwa kimiani na Justin Omary aliyepachika mabao mawili dakika ya 2 na 27, Omary Kanyoro alipachika bao moja dakika ya 39 na mawili mengine yalipachikwa na Khamis Mcha dakika ya 46 na 50 ya mchezo.
"Tunawashukuru mashabiki kwa sapoti kubwa ambayo wanatupa hiyo ni furaha kwetu na malengo yetu ni kuona kwamba tunapiga hatua kubwa zaidi ya hapa," alisema Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji, Fortunas Johnson.
Kupitia Ukurasa wao rasmi wa Istagram Dodoma Jiji wameandika kuwa "Tunaomba radhi mashabiki wetu kwa ushindi mwembamba siku ya leo, kikubwa tumefuzu hatua inayofuata".
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.