Jiji la Asili ni mradi unaolenga kuonyesha uthamani wa uoto wa asili mjini. Mradi huu unahusisha mikoa minne (4) nchini Tanzania ambayo ni Dar es salaam , Arusha , Kilimanjaro na Dodoma. Mikoa hii imechaguliwa kuwa sehemu ya kwanza ya mpango huo ili kuwafanya watu wawe na uelewa juu ya uoto wa asili mijini.
Mradi huu wa Jiji la Asili ulianzishwa na kampuni ya ICLEI mwaka 2017 na utadumu hadi 2020 ukiungwa mkono na Serikali ya awamu ya tano kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI). Jijini Dodoma wanaosimamia mradi huu ni BORDA na taasisi ya NIPE FAGIO .
Taasisi hizi za mazingira zimeshirikiana kutekeleza ufungwaji maji kijivu katika eneo la wazi la Nyerere Square na kuboresha bustani hiyo yenye uoto wenye mimea tofauti tofauti na inaruhusu kila raia kutembelea kupumzika na kuingiliana na viumbe hai kama vipepeo na wengine wazuri, zaidi ya hayo ni kuongeza uelewa juu ya utunzaji wa mazingira.
Akipongeza tukio hilo la kuboresha eneo la wazi la Nyerere Square Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe amesema kuwa kwa niaba ya Halmashauri na wananchi wa jiji la Dodoma tunashukuru sana kwa kutuonyesha mfano jinsi gani tutunze mazingira yetu . hivyo watu wote wazee, vijana na watoto mazingira yanawahusu kwa hivyo maendeleo ya miji yetu yanatuhusu sisi sote.
Aidha alimalizia kwa kusema wananchi tutengeneze bustani na tuzitunze ili tuache sehemu ya mji kupumua pia vyombo vya habari na wana habari muwe washawishi wakubwa wa utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa misitu ili mjini kubaki na uoto asili na kuwa mahali pakuvutia alisema Prof. Mwamfupe
Mhandishi mradi wa taasisi ya BORDA Charles Mhamba alisema kuwa mradi huu unaendeshwa na maji ya kunawia mkono katika choo chetu cha hapa hapa Nyerere square na pia maji haya yanaweza kukuza nyasi na miti kama mizabibu ambayo pia tumepanda hapa ili kutengeneza kivuli cha asili hapo baadae.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.