Na Sofia Remmi.
Habari-Dodoma Rs.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Jabir Shekimweri amewapongeza Benki ya NBC kwa kutambua na kuunga mkono Jitihada ya Mhe.Rais.
Mhe. Shekimweri ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya ugawaji wa pikipiki kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Jengo la Mkapa.
Akizungumza katika Hafla hiyo Mhe.Shekimweri amesema kuwa mara ya sita NBC wamekuwa wakifanya Marathon katika Mkoa wa Dodoma.
Amesema mwaka 2025 Marathon imelenga kuokoa maisha ya mama na watoto na kufanya Mbio hizo kuwa za Kimataifa zaidi kwasababu Mataifa Mbalimbali yanakuja kushiriki .
"Niwapongeze kwani Mbio hizo zimeunganishwa na ajenda za Kitaifa katika kuunga Mkono Jitihada za Mhe.Rais masuala ya Afya katika kuongeza zaidi bajeti ya afya na ununuzi wa Dawa kwa upande wa NBC Mmeunga Mkono katika masuala mazima ya usonji na kansa ya shingo ya kizazi”
Aidha Mkurugenzi wa wateja wakubwa benki ya NBC Bw.Elvis Ndunguru amesema NBC Marathon imeamua kuchangia pikipiki 10 zenye thamani ya shilingi Milioni 28 kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma.
Amesema NBC marathon imesaidia kuchangia mchango wa Mama na Mtoto kwa kupima saratani ya shingo ya Kizazi,kutoa elimu kwa wakunga katika hospitali na kupambana na ugonjwa wa usonji.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.