Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kanda ya kati imetembelea makundi mbalimbali ya jamii na kutoa elimu juu ya upandaji wa miti majumbani kwa ngazi ya familia, wafanyabiashara na taasisi mbalimbali .
Kampeni hiyo ya kutoa elimu ya upandaji miti majumbani imefanyika maeneo ya Area C, Soko la majengo, na Msalato ikiwa imebeba kauli mbiu ya “Dodoma ya kijani inawezekana” elimu hiyo ilikuwa imebeba makundi ya sanaa mbalimbali nyimbo, sarakasi na maigizo yenye lengo la kufikisha ujumbe katika jamii
Afisa Mazingira Ally Mfinanga aliwasisitiza wananchi kupanda miti isiyopungua mitano kwa ngazi ya familia, miwili ya kwa ajili ya kivuli na mitatu ni miti ya matunda. Aliwaelezea wananchi faida kubwa za miti kwa kizazi kilichopo na kijacho. Moja ya faida kubwa ikiwemo kuleta mvua.
“wananchi kwa pamoja tukishirikiana kupanda miti mitano kwa kila nyumba miti hiyo miwili kwa ajili ya kivuli na miti mitatu iwe ya matunda lakini pia tukiweza kufanikisha zoezi hili kila mmoja wetu akapanda miti ina faida nyingi sana haswa katika maisha yetu wanadamu, kutengeneza kivuri, huleta hewa safi, lakini pia miti huleta mvua, jamani Dodoma hapa mvua zinachelewa sana. Sasa hivi mikoa mingine mvua zinanyesha, Dodoma ya kijani inawezekana “ alisema kwa msisitizo Mfinanga.
Mfinanga alitoa maelekezo ya utaratibu wa namna ya kupata miti hiyo kwa upande wa taasisi, shule, msikitini, kanisani, Hosptali na kwa mwananchi wa kawaida kama ataitaji miti isiopungua mitano wafike ofisi za Halmashauli ya Jiji watapewa miti bure bila gharama yoyote. Kwa wale wanaohitaji miti ambayo watapanda majumbani kwao, basi waweze kununua katika vitalu mbalimbali vilivyopo katika Jiji la Dodoma.
Kikundi cha utamaduni kikitumbuiza kwenye kampeni ya upandaji miji Jijini Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.