MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amefanya Mkutano na waandishi wa Habari kutangaza matokeo ya darasa la Saba kimkoa pamoja na Mkakati kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2024. Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa shule ya msingi St. Gaspar iliyopo Miyuji Jijini Dodoma.
Senyamule amebainisha matokeo hayo kwa kila Halmashauri ya Mkoa wa Dodoma na akionesha ongezeko la ufaulu lililopatika.
"Mkoa una ufaulu wa asilimia 87.05 mwaka 2023 sawa na ongezeko la asilimia 4.04 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2022 ambapo ufaulu ulikua asilimia 83.01. Katika matokeo haya, kila Halmashauri imeongeza ufaulu. Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa imepanda kutoka 78% - 86% sawa na ongezeko la 7.91% Wilaya ya Kondoa kutoka 71.50% hadi 78.02 sawa na ongezeko la 6.52%.
"Chemba imetoka 70.53% hadi 75.49 sawa na ongezeko la 4.96, Chamwino kutoka 86.49% hadi 89.81 sawa na ongezeko la 3.32%, Jiji la Dodoma kutoka 89.93% hadi 93.18% sawa na ongezeko la 3.25%, Kondoa Mji kutoka 86.28 hadi 88.37% sawa na ongezeko la 2.09%, Bahi kutoka 95.88% hadi 97.64% sawa na ongezeko la 1.76% na Mpwapwa kutoka 83.91% hadi 84.56% sawa na ongezeko la 0.65. Hii ni hatua kubwa kwa Mkoa wetu". Amesema Senyamule
Aidha amewataka wazazi kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2024 wanakwenda shule kwani bila kufanya hivyo adhabu kali itatolewa kwa wanafunzi wote watakaobainika.
"Kufuatia matokeo hayo, jumla ya wanafunzi 52,891 wamefaulu ikiwa wavulana ni 22,893 na wasichana ni 29,998 sawa na 87.05% ya wanafunzi waliofanya Mtihani 2023. Wanafunzi wote waliofaulu wamepangiwa shule katika awamu ya kwanza. Hakuna Mwanafunzi aliyefaulu na hajapangiwa shule katika Mkoa wa Dodoma.
"Naagiza wanafunzi wote wawepo darasani ifikapo tarehe 8 Januari, 2024 bila kukosa. Kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo, tumeweka Mkakati kuhakikisha wanarudi shuleni kwani Mkoa hautalifumbia macho suala hilo. Wale ambao hawatakua darasani kufikia tarehe 8, bila sababu za msingi, watapewa adhabu ya kulima matuta 10 kama utekelezaji wa Mpango wa Elimu ya kujitegemea" Ameongeza Senyamule.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.