Uongozi wa Mkoa wa Dodoma umewazawadia kwa kuwalipia ada ya miaka 2 yaani kidato cha tano na cha sita wanafunzi wote waliofaulu mitihani ya kidato cha nne kwa kupata Daraja la Kwanza Pointi 7 kutoka katika Shule za Serikali na Wasichana wote waliofaulu Daraja la Kwanza kwa kupata pointi 7, 8 na 9 kutoka Shule za serikali.
Aidha, “Tumewazawadia walimu wote ambao walifaulisha kwa alama A katika masomo yao kwenye mitihani ya kidato cha nne, vile vile tumezawadia Shule zote za msingi za serikali ambazo zimetoa watoto waliofaulu Kidato cha kwanza kwenda shule za wenye vipaji Maalumu.
"Tumeianza safari ya kuijenga Elimu ya Mkoa wetu, naamini mwakani tukijaaliwa tutakuwa na maboresho mengi, makubwa na mazuri katika kumotisha walimu na wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari.” Alisema Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka.
Mkuu huyo wa Mkoa hakuacha kuwapongeza wadhamini waliohusika katika shughuli na tuzo hizo ambao ni NMB, CRDB, TCB, NBC, EXIM, PBZ, EWURA, DUWASA, RUWASA, TARURA, TANESCO, TANROAD na Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mwisho aliwapongeza pia viongozi wa Dini, vyama vya siasa, machifu na wazazi wote kwa kuunga mkono suala la uendelezaji na kukuza elimu mkoani Dodoma. “Hongereni sana wazazi na walimu wetu” alimalizia Mtaka.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.