TAASISI ya Maendeleo ya Vijana Mkoani Dodoma (DOYODO) imewasilisha Ripoti ya Miaka Miwili ya utekelezaji Mradi wa 'MAGAUNI MANNE' unaolenga kutokomeza mimba za utotoni kwa mabinti wa Shule kwenye kata nne Jijini Dodoma ambazo ni Miyuji, Chang'ombe, Mnadani na Nzuguni, hafla iliyofanyika Alhamisi tarehe 2 Septemba, 2021.
Mgeni Rasmi wa hafla hiyo Naibu Waziri Kazi, Vijana na Ajira Mh. Patrobas Katambi alitoa kongole na kuwapongeza Shirika la DOYODO na DSW kwa ushirikiano katika kuhakikisha huduma rafiki za Afya ya uzazi kwa vijana zinaboreshwa ili kupunguza tatizo la mimba za utotoni ambalo limekuwa kikwazo kwa mabinti wengi kushindwa kutimiza ndoto zao na kupelekea kupoteza nguvu Kazi ya Taifa.
Akihitimisha uwasilishaji wa ripoti hiyo Mkurugenzi wa DOYODO Rajabu Suleiman aliisema kauli mbiu ya mradi huo kuwa "Dodoma bila mimba za utotoni inawezekana" huku akirejea kauli ya Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa 'Kazi Iendelee' kudhihirisha kwamba taasisi hiyo bado inaendelea na mradi huo unaosaidia mabinti wengi kupata elimu na uelewa utakaowasaidia kutimiza ndoto zao za mafanikio katika masomo na maisha yao ya kila siku.
Chanzo: Idara ya Habari na Mawasiliano Ya Kidijitali DOYODO
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.