TAASISI ya Maendeleo ya Vijana mkoani Dodoma (DOYODO) imepongezwa kwa kuwakutanisha wadau na kuweka mikakati ya pamoja ya kutokomeza mimba za utotoni jijini Dodoma.
Pongezi hizo zilitolewa na Mgeni rasmi Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Sharifa Nabalang'anya (aliyesimama pichani juu) ambaye pia alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau kuendelea kushirikiana na viongozi wa Serikali katika kuchochea maendeleo ya vijana wa jiji Dodoma.
Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Vijana mkoani Dodoma (DOYODO) kupitia mradi wa magauni manne uliwakutanisha wadau wa afya ya Uzazi kwa vijana jijini Dodoma (Dodoma SRH-allies) na baadhi ya viongozi wa Serikali kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakiwemo Katibu wa Afya wa Jiji, Mratibu wa Huduma rafiki na wakuu wa vituo vya Afya vya Jiji la Dodoma.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa DOYODO Rajabu Juma Suleiman alitoa shukrani zake za dhati kwa wadau wote walioshiriki mkutano huo muhimu na aliahidi kuendelea kuchapa kazi kwa maendeleo ya vijana wa Dodoma.
DOYODO ni taasisi ya vijana yenye nguvu inayoendeshwa na vijana kwa mafanikio makubwa katika kuinua hali ya uthubutu na uchumi wa vijana jijini Dodoma na Tanzania kwa ujumla.
Katibu wa Afya wa Jiji la Dodoma Habiba Thabit (aliyesimama) akichangia mada kwenye mkutano wa wadau wa afya ya Uzazi kwa vijana jijini Dodoma mkutano ulioandaliwa na DOYODO.
Mratibu wa Huduma rafiki kutoka Jiji la Dodoma Bi. Lona (aliyesimama kulia) alipokuwa akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa mkutano wa wadau wa afya ya uzazi kwa vijana jijini Dodoma.
Chanzo: Idara ya Habari na Mawasiliano - DOYODO
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.