NAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Mhe. Emmanuel Chibago amewaomba wadau wa mazingira kuiga mfano wa kutunza mazingira uliofanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) wakishirikiana na benki ya Equity kwa kuboresha mzunguko wa magari eneo la Makole jijini hapa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mzunguko wa Makole (round about) amewaomba wadau wengine wote wa mazingira kuiga mfano huo ili kuboresha mandhari ya Jiji la Dodoma na mazingira yake.
Chibago aliwataka wadau wote wa mazingira kufanya ili kuunga mkono taasisi hizo mbili zilizoonesha mfano bora wa kutunza mazingira na kuboresha miundombinu ya mazingira kwa sababu italeta muonekano mzuri jijini hapa.
“Nianze kwa kuwapongeza sana mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mjini Dodoma na ‘Equity bank’ kwa kuonesha mfano huu mkubwa wa jinsi gani tunavyoweza kutunza mazingira na tukaleta muonekano mzuri. Hivyo, niwaombe wadau wengine wote wa mazingira jijini kwetu Dodoma kuunga mkono juhudi hizi” alisema Chibago.
Aidha, kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Maji-taka (DUWASA) jijini Dodoma, Mhandisi Kashinga Yunga, kwa kushirikiana na benki ya Equity wameandaa utaratibu utakao wasaidia watu wa hali ya chini kukopeshwa fedha ili waweze kuunganishiwa huduma ya maji safi na maji taka jijini hapa.
“Tumezindua muungano huu kuwawezesha wateja wetu ambao wanaitaji kupata huduma ya maji safi na maji taka lakini hawana uwezo wa kulipia ghalama za kutengeneza miundombinu hiyo.
“Wenzetu ‘Equity Bank’ wametushika mkono kwa kutoa mikopo hiyo midogo midogo wakiwa na lengo la mtu asikose maji au huduma ya majitaka kwa sababu hana fedha wakati huo” alisema Yunga.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Equit Mkoa wa Dodoma, Joseph Malatuna amesema lengo la mkakati huo ni kutoa suluhisho endelevu la kudumu kupitia uwezeshaji kwa jamii kupitia mikopo midogo midogo katika sekta ya maji ili kuhakikisha mwananchi mmoja moja au kikundi wanapata huduma za maji safi na usafi wa Mazingira.
“Tupo katika kushirikiana na wenzetu DUWASA, tunaelekeza nguvu zote kwa pamoja katika upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira hii ni kuendana na lengo la DUWASA na lengo letu kutoa suluhisho endelevu la kudumu kupitia uwezeshaji kwa jamii kupitia mikopo midogo midogo katika sekta ya maji na kuhakikisha mwananchi mmoja moja au kikundi wanapata huduma za maji safi na usafi wa Mazingira” alisema Malatuna.
Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Mhe. Emmanuel Chibago (wa tano kulia) akiwa na viongozi wa DUWASA, Equit Bank na Jiji la Dodoma baadha ya kuzingua eneo la mzunguko lililoboreshwa na DUWASA na Benki ya Equit.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.