MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini (DC), Jabir Shekimweri ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA), kwa kuongeza makusanyo ya mwezi kutoka shilingi Bilioni 1.3 mpaka shilingi Bilioni 1.8.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki (Ijumaa ya tarehe 20 Agosti, 2021) wakati alipokuwa akifungua semina ya Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliyoandaliwa na DUWASA.
Pia, aliwataka kuendelea kuchukua hatua katika maeneo mengine ikiwemo upotevu wa maji kutoka asilimia 30 kushuka zaidi.
“Matarajio yangu kila hatua ya elimu mnayotoa ikikamilika, mrejesho mnaoupata kwa wateja mtautumia vizuri na kutoa mkakati wa kuimarisha huduma” alisema Shekimweri.
Alisema umuhimu wa semina hii ni kuweka msingi mzuri wa ushirikiano baina ya DUWASA, madiwani na kuwa na msimamo wa pamoja katika kumuhudumia mwananchi.
Alisema imekuwa dhamira ya siku nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye ameongeza bajeti kubwa sana kwenye bajeti ya maji ili kumtua mama ndoo kichwani.
Wakati akijibu maswali kutoka kwa Madiwani, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph alisema kufungwa kwa wateja ili mita hizo bado zina changamoto mbalimbali.
Hata hivyo, amesema Wizara imewapa maelekezo ya kufanya majaribio ya mita mbalimbali kutoka kwenye makampuni tofauti ili kupata mita zenye ufanisi.
Mita hizo zinagharama kubwa ambapo mita moja inauzwa kati ya shilingi laki tatu na hamsini elfu mpaka laki nne.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.