BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma limefanyika leo 29 Aprili, 2021 katika mkutano wake wa kawaida kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa shughuli kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2020/2021 ya Halmashauri hiyo.
Akifungua mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, Mwenyekiti wa baraza la hilo ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe aliwakaribisha wajumbe na viongozi wote huku akisema kuwa “karibuni katika mkutano huu muhimu tujadili maslahi ya watu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kama apendavyo Mwenyezi Mungu na siyo kama tupendavyo sisi” alisema Prof. Mwamfupe.
Wakichangia masuala yanayohusu maendeleo ya sekta ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji hilo, wajumbe wa Baraza hilo lenye Kata 41 na Madiwani 60, walisema kuwa uboreshwaji wa elimu uwe kipaumbele katika Halmashauri Jiji la Dodoma.
Akijibu hoja za wajumbe hao juu ya maendeleo ya elimu, Katibu wa mkutano huo, Wakili Msekeni Mkufya alisema kuwa Halmashauri imeweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu.
“Tunatumia mbinu nyingi kuboresha sekta ya elimu hapa kwetu na kiujumla miundombinu ya elimu ni kipaumbele kwetu. Hakuna siku tutafikia hatua kuwa tusahau madarasa, tusahau madawati, sijui kama itawezekana sababu kwetu ni kipaumbele na Dodoma inakuwa kwa kasi pia vitu vingi vinaendelea“ amesema Wakili Mkufya.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.