Na. Coletha Charles, Dododma
Wakazi wa Kata ya Mkonze Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamewezeshwa mafunzo ya Ukatili wa Kijinsia, Ukatili dhidi ya watoto, Ukatili wa Kiuchumi na Mikopo ya Asilimia kumi katika Shule ya Msingi Mkonze.
Akiwezesha mafunzo hayo, Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Mkonze, Noela Wilered, alisema kuwa wanatoa elimu ya Ukatili wa kijinsia na Ukatili dhidi ya watoto kwa wananchi ili kupunguza matukio ya ukatili ngazi ya mkoa na taifa.
“Ukatili wa kimwili na wa kingono unaongoza hasa kulawitiwa kwa watoto. Niwaombe wazazi tunatakiwa tuwe waangalizi na walezi wa watoto katika makuzi ili waweze kuwa wawazi waeleze changamoto wanazokumbana nazo. Lakini pia wazazi msiwe wakali kwa watoto hadi wawaogope” alisema Wilered.
Aidha, Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Mkonze, Theresia Camilius, alitoa elimu ya mikopo ya asilimia kumi 4.4.2 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili kukunza uchumi wao na namna ya kuweka akiba. Pia Muelimishaji Mradi wa Ahadi Kata ya Mkonze, Happiness Simon, aliutambulisha mradi huo na watendaji kazi wake kwa wananchi waweze kuwatambua Baba Bora na kuweza kushirikiana nao katika malezi na kuelimisha Jamii.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.