Na. Dennis Gondwe, DODOMA
FAMILIA nchini zimetakiwa kupanda miti ili kuunga mkono juhudi za serikali za kukijanisha Tanzania kwa kuhakikisha mazingira bora na salama.
Kauli hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea na mamia ya wananchi waliojitokeza katika zoezi la upandaji miti lililofanyika katika shule ya msingi Msalato ikiwa ni maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Dkt. Mpango alisema kuwa kila familia lazima ipande miti angalau mitatu, miti miwili ya matunda na mti mmoja wa kivuli. Alisema kuwa miti hiyo ni muhimu na itawasaidia watoto kuwa na utamaduni wa kupenda mazingira.
Aidha, alivitaka vituo vyote vya mafuta vipande miti na kuitunza katika maeneo yao. “Vilevile, kampuni zinazofyatua matofali wapewe hata nusu kilometa ili wapande miti” alisema Dkt. Mpango.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alisema kuwa katika maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar itapandwa miti 1,000 katika shule ya msingi Msalato. “Mheshimiwa Makamu wa Rais, shule hii tuliihamisha kupisha upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Msalato. Shilingi milioni 437.6 zililipwa kama fidia. Shule ina eneo la ekari 6.2 ikiwa na jumla ya wanafunzi 1,116.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.