• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Fanyeni kazi kwa faida - Chongolo

Imewekwa tarehe: June 26th, 2023

Na. Dennis Gondwe, NALA

WAFANYAKAZI wa Kiwanda cha Mbolea cha Itracom wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kujipatia maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo alipokuwa akiongea na wafanyakazi wa Kiwanda cha Mbolea cha Itracom kilichoko katika Kata ya Nala Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

“Kwa wafanyakazi hongereni kwa kazi. Mmepata fursa ya kufanya kazi, mfanye kazi kwa kujituma, uadilifu na uaminifu. Mjitume kutafuta tija ambayo inatakiwa kwa pande zote, kwa muwekezaji na kwetu sisi wafanyakazi. Huwa tunafikiri kinapoharibika, kinaharibika cha mwingine na sisi tunabaki salama. Lakini kikiharibika sisi ndiyo wa kwanza kupata madhara. Mimi ndiyo wa kwanza kukaa nyumbani kisha mwekezaji ndo anafuata kutegemea na aina ya hasara. Tufanye kazi kwa moyo ili kulinda ajira zetu lakini tujitume zaidi ili waongeze mishahara. Tujiepushe na udokozi” alisema Chongolo.

Katibu Mkuu Chongolo aliitaka menejimenti ya kiwanda hicho kuwekeza kwenye utafiti. “Niwaombe sana kuwekeza kwenye utafiti wa udongo wetu kwa kulinganisha na mbolea mnayozalisha ili tija tunayoanza kutangaza sasa iwe endelevu. Tija hiyo iwe ya muda wote kuliko baadae ije kuonekana na changamoto kwenye baadhi ya maeneo” alisema Chongolo.

Akiongelea changamoto ya Maji inayowakabili wakazi wa Kata ya Nala, alisema kuwa ufumbuzi utafutwe kupitia mpango wa Maji unaopelekwa katika kiwanda hicho. “Mpango wa kupeleka Maji kiwandani lazima uende sambamba na kutoa huduma hiyo kwa kiwanda na wananchi pia. Tukipeleka Maji kwenye kiwanda pekee hata kama ni mimi ningelalamika. Ndiyo ukweli na tukipeleka kwa wananchi na kiwandani hakuna maji maana yake tija hatuwezi kuipata kwa wakati. Ni lazima twende kwa kuangalia pande zote. Kwenye uwekezaji wa namna hii ni lazima wataalam wetu wawe wanajua kuweka usawa wa vitu hivi ili wananchi wasimchukie muwekezaji kwa sababu ya matatizo yetu ya kuwanyima huduma.

Katibu Mkuu wa CCM taifa alifanya ziara katika Wilaya ya Dodoma, alitembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani hapo.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.