OFISI ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inaendelea kuwakumbusha watumishi wanaohusika katika kuandaa taarifa na kuomba vitendanishi vya maabara kufanya maoteo kwa usahihi na kuomba vitendanishi hivyo kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa Bungeni Novemba 11,2022 na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, David Silinde wakati wa kujibu swali la msingi la Shamsia Mtamba Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, lililouliza Serikali ina mpango gani wa kusambaza vipimo vya maabara hasa vipimo vya Maralia katika Zahanati za Mtwara Vijijini.
Akijibu swali hilo Silinde amesema hali ya upatikanaji wa vitendanishi wa vipimo vya Maralia katika Kanda ya Mtwara hadi kufikia Octoba 2022 ni vitepe 631,825 ukilinganisha na matumizi ya vitendanishi hivyo ambavyo ni 84,150 kwa mwezi hivyo kuna shehena ya vitendanishi vya kutosheleza miezi saba ijayo.
Kabla ya kufika tarehe 30 Desemba 2022 Bohari Kuu ya Dawa inategemea kupokea shehena nyingine ya vitendanishi vya Maralia" amesema Silinde
Aidha katika swali lake la nyongeza Shamsia aliuliza, Serikali haioni umuhimu wa kusambaza vipimo vikubwa kwenye Zahanati za Mtwara Vijijini na Hospitali ya Wilaya ya Nanguruwe ili kuweza kupima magonjwa mengine.
Akijibu swali hilo, Silinde amesema umuhimu wa kuongeza vipimo vikubwa upo na ndio kazi anayofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya inatarajia kupokea Shilingi bil. 169.7 kutoka Banki ya Dunia kwaajili ya ununuzi wa vifaa, vifaa tiba na vitendanishi kwaajili ya maabara.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.