Na. Dennis Gondwe, Ipagala-DODOMA
KIKUNDI cha Wanawake cha ufugaji kuku Winning Star kilichokopeshwa shilingi 20,000,000 fedha ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kimetakiwa kufanya marejesho yake mapema ili kiendelee kuaminika na kuwezesha wananchi wengine kupata mkopo.
Agizo hilo lilitolewa na Diwani wa Kata ya Nkuhungu, Daud Mkhandi alipoongoza timu namba mbili ya Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kutembelea na kukagua shughuli za kikundi hicho kilichopo katika Kata ya Ipagala.
Mkhandi alikiagiza kikundi hicho kurejesha mkopo wake kwa mujibu wa mkataba ili kuwawezesha wananchi wengine kukopa pamoja na kuongeza wigo wa kukopeshwa tena kitakapohitaji mkopo mwingine. Kikundi hicho kilishauriwa kuwasilisha ombi la kutafutiwa eneo la kufanyia shughuli zao katika halmashauri tofauti na kutegemea eneo la kupanga.
Akiwasilisha taarifa fupi ya kikundi cha wanawake cha Winning Star Mjumbe wa kikundi hicho, Julia Malaba alisema kuwa kikundhi hilo kinalenga kuwa ni wafugaji wakubwa wenye weledi wakifanya ufugaji unaoendana na teknolojia ya kisasa. “Kikundi kinalenga kupunguza utegemezi katika familia na jamii na kujiimarisha kiuchumi” alisema Malaba.
Ikumbukwe kuwa kikundi cha Winning Star ni kikundi cha wanawake sita wajasiriamali kinachojihusisha na ufugaji wa kuku, uuzaji wa kuku na mayai kilichoanzishwa tarehe 10 Desemba, 2020.
=30=
Kamati ya Fedha yaridhishwa mradi shamba la zabibu
Na. Dennis Gondwe, Msalato- DODOMA
KAMATI ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma yaridhishwa na mradi wa shamba la zabibu la halmashauri na kuelekeza juhudi ziongezwe ili uzalishaji uongezeke na kuakisi thamani ya fedha.
Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Kata ya Nkuhungu, Daud Mkhandi alipoongoza timu namba mbili ya Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kutembelea na kukagua mradi wa shamba la zabibu la halmashauri katika Kata ya Msalato.
Mkhandi alisema kuwa Kamati ya Fedha na Utawala imeridhishwa na hali ya shamba hilo na kuipongeza Divisheni ya Kilimo mjini kwa kuanzisha na kusimamia shamba darasa hilo.
…
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.