NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – Mhe. Zainabu Katimba amewaelekeza wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanafanya tathimini ya miundombinu na thamani chakavu kwenye shule za Msingi na Sekondari.
Pia amewaelekeza kutenga Bajeti kutoka katika Mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya Ukarabati wa Miundombinu mbali mbali kama vile Matundu ya Vyoo, Madawati, Viti na Meza.
Mhe. Katimba amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Mhe. Anna Kilango Malecela (Mb) aliyetaka kujua, Je serikali ipo tayari kutoa maelekezo kwa Halmashauri ya Tarime kuondoa changamoto ya Matundu ya Vyoo, Madawati, Viti na Meza. Swali alilouliza kwa niaba ya Mbunge wa Tarime vijijini Mhe. Mwita Waitara(Mb) katika kipindi cha Maswali na Majibu.
“Wajibu wa kutunza na kusimamia Shule uko chini ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Tafrisi yake ni kwamba ununuzi wa Madawati, Viti Ujenzi wa Matundu ya vyoo, ujenzi wa Madarasa na Miundombinu mingine ni wajibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia Bajeti za Maendeleo kwahiyo nichukue nafsi hii kuwaelekeza Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanafanya Tathimini ya Miundombinu hiyo” Mhe. Katimba.
Pia Mhe. Katimba amesema mkakati wa serikali ni kumaliza changamoto ya Madawati Nchini kwa kuhakikisha kwamba kila Darasa jipya linalojengwa linawekewa Madawati kumi na tano, yaani Dawati moja kwa Wanafunzi watatu kwa Shule za Msingi na Viti hamsini na Meza hamsini kwa shule za Sekondari kote Nchini
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.