Faru mweusi anayeaminika kuwa mkongwe zaidi duniani amekufa nchini Tanzania akiwa na umri wa miaka 57, kulingana na mamlaka ya Ngorongoro ambapo mnyama huyo alikuwa akiishi.
Faru huyo jike, anayeitwa Fausta, alikufa kwa sababu ya kuaminika kuwa ya asili mnamo Disemba 27 mahali maalum alipokuwa akitunzwa, baada ya kuishi maisha yake kwa kipindi kirefu porini, Mamlaka ya Uhifadhi wa Ngorongoro ilisema katika taarifa yake Jumamosi.
"Rekodi zinaonyesha kuwa Fausta aliishi kwa muda mrefu zaidi ya wanyama wowote ulimwenguni na alinusurika kwa kuishi huko Ngorongoro, katika kipindi ambapo uwindani ulikuwa ni buru kwa zaidi ya miaka 54" kabla ya kuhamishwa na kutunzwa mahali maalum mnamo 2016, ilisema taarifa hiyo.
"Fausta kwa mara ya kwanza alionekana katika eneo la Ngorongoro mnamo 1965 na mwanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, akiwa na umri wa kati ya miaka mitatu na minne. Afya yake ilianza kudhoofika mwaka wa 2016, wakati tulipolazimika kumweka na kumhifadhi mahali maalum, baada ya mashambulio kadhaa kutoka kwa fisi na majeraha makubwa" iliongeza taarifa hiyo.
Sana, faru mweupe wa kike wa kusini, mwenye umri wa miaka 55, alichukuliwa kama faru mzee kabisa duniani wakati alikufa akiwa eneo maalum katika uwanja wa kufugia wanyama wa Planète Sauvage huko Ufaransa, mnamo 2017.
Mamalaka ya uhifadhi ya Ngorongoro inakadiria miaka ya kuishi ya faru kuwa kati ya miaka 37 hadi 43 wakiwa porini, wakati wanaweza kuishi hadi wazee zaidi ya miaka 50 wakifungiwa na kutunzwa sehemu maalum.
Chanzo: The Guardian
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.