SHULE ya msingi Chihoni imetakiwa kuwekeza katika michezo ili kuibua vipaji, kuchochea ufaulu na kuondoa utoro kwa wananfunzi.
Kauli hiyo ilitolewa na mgeni rasmi katika mahafali ya darasa la saba Meneja mradi wa Mkoa wa Dodoma kutoka mradi wa Tuimarishe Afya -Health Promotion System Strengthening (HPSS), Kenneth Gondwe katika hotuba yake iliyosomwa na Dennis Harrison katika mahafali hiyo.
Gondwe alisema kuwa michezo ni mizuri kwa kuimarisha afya ya mwili na akili. Aliushauri uongozi wa shule hiyo kupanga ratiba itakayowezesha wanafunzi kushiriki katika michezo mbalimbali kwa lengo la kuwajengea kujiamini na kudumisha urafiki miongoni mwao. Michezo inasaidia kujenga na kuibua vipaji vya wanafunzi, aliongeza. Alisema kuwa kupitia michezo, vijana wamejitengenezea nafasi za ajira na kuondokana na tatizo la kusubiri kuajiriwa.
Katika kuonesha umuhimu wa michezo kwa wanafunzi wa shule hiyo, aliahidi kuwatafutia mipira kwa ajili ya mchezo wa soka na netiboli. Aidha, alisema kuwa atamshirikisha diwani wa kata husika kuona uwezekano wa kuwatafutia jezi.
Katika risala ya wanafunzi wahitimu iliyosomwa na Sophia Julius alisema kuwa pamoja na elimu waliyopatiwa shuleni hapo, shule inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa vya michezo. Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni mipira kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu na netiboli na sare za michezo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.