• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Fursa ya Ufugaji wa Mbwa katika Jiji la Dodoma

Imewekwa tarehe: August 3rd, 2025

Na Eupilio Anthony, DODOMA

Maonesho ya sherehe za wakulima nchini inazofahamika kama Nanenane, wananchi wajitokeza kujionea mifugo, bidhaa za kilimo, uvuvi na bidhaa zilizosindikwa na wajasiliamali kutokana na mazao hayo huku wakifurahishwa na ufugaji wa mbwa kisasa.

Moja kati ya wafugaji na mfanyabiashara wa mbwa, Mwakaleli Mwakasege aliwaeleza wananchi anavyofanya biashara hiyo. “Mimi ni mfugaji wa mbwa kwa zaidi ya miaka 10 na leo kwenye sherehe hizi za Nanenane nimefurahi sana kuona jamii inaanza kutambua thamani ya mnyama huyu. Mbwa si tu mnyama wa kufuga kwa ajili ya ulinzi ni rafiki mkubwa wa familia, mlinzi wa mali, na kwa sasa, chanzo cha kipato kwa watu wengi kama mimi” alisema Mwakasege.

Aliendelea kueleza tabia za mbwa anapoishi na binadamu kuwa yapo mambo akifundishwa anaelewa. “Mbwa anaweza kufundishwa tabia mbalimbali, anayo akili ya haraka, na ni mnyama mwenye hisia anajua kufariji, kulinda na pia kusaidia kwenye shughuli za kila siku. Wapo wanaotumia mbwa kusaidia watu wenye ulemavu, wengine kwenye utafutaji wa watu waliopotea, hata kwenye kilimo na usalama wa mashamba” alieleza Mwakasege.

Kwa upande wa kiuchumi alieleza namna ufugaji wa mbwa una faida katika kukuza kipato. “Ufugaji wa mbwa unaweza kugeuka kuwa biashara yenye faida kubwa. Mbwa wanaofugwa vizuri kwa kupewa chanjo, chakula bora, na mafunzo huuzwa kwa bei nzuri, na pia huduma zao za ulinzi hugharamiwa” alieleza huku akitabasamu Mwakasege.

Aidha, alitoa rai kwa watanzania kujishughulisha na ufugaji wa mbwa huku akichagiza kwa kutumia msemo wake kwamba “ Tumchukulie mbwa kama sehemu ya maendeleo ya familia na uchumi wetu, ana thamani kubwa kuliko tulivyozoea kufikiri” alisema Mwakasege.

Kwa upande mwingine, Mtaalam na Mfugaji wa Mbwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Anthony Massawe alisema kuwa amekuwa mfugaji wa mbwa kwa zaidi ya miaka nane na ameona umuhimu katika maonesho ya Nanenane kuwapa wananchi elimu na umuhimu wa kufuga mbwa kwa tija. “Kwanza kabisa, watu wengi hudhani kwamba mbwa anakula chochote, hili halina kweli. Ili mbwa awe na afya njema, awe mkakamavu, mwenye kinga dhidi ya magonjwa na aweze kutimiza majukumu yake kama ulinzi au kuwa rafiki wa familia anapaswa kulishwa lishe kamili yenye virutubisho vyote muhimu. Mbwa anahitaji mlo wenye protini kama nyama au dagaa, wanga kama wali, viazi au dona, mboga kwa ajili ya vitamini, pamoja na maji safi ya kutosha kila siku. Mbwa pia hapaswi kufungiwa bila nafasi ya kutembea au kufanya mazoezi. Anahitaji mazingira safi, yenye nafasi ya kutosha na mahali pa kujisitiri wakati wa mvua au jua kali” alisema Massawe.

Alimalizia kwa kutoa shukrani kwa serikali na waandaaji wa maonesho ya Nanenane. “Ningependa kutoa shukrani za dhati kwa waandaaji wa maonesho haya ya Nanenane, kwa kunipa nafasi ya kuweka banda la mbwa. Sherehe hizi zimekuwa jukwaa muhimu sana la kuelimisha, kuhamasisha na kuunganisha wafugaji, wakulima na wataalamu kutoka kila pembe ya nchi yetu pia tunapata fursa ya kushiriki na kuchangia elimu kuhusu ufugaji” alisema Massawe. 



Imehaririwa na Nancy Kivuyo








Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Serikali yaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza- Mwambene

    August 18, 2025
  • Afisa elimu mkoa wa Dodoma akagua maandalizi ya Juma la elimu ya watu wazima

    August 17, 2025
  • Wafanyabiashara wa mkoa wa Dodoma watangaziwa fursa za biashara nchini indonesia

    August 16, 2025
  • Wafugaji waaswa kufuga kwa kuzingatia uwezo wa malisho ili kupata tija

    August 15, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.