GHARAMA nafuu za data kwenye simu ni miongoni mwa mafanikio ambayo tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye upatikanaji wa gharama nafuu. Imeelezwa kuwa uwekezaji kwenye Miundombinu na Sera nzuri ya Serikali kwenye Sekta ya Mawasiliano zimewezesha upatikanaji wa huduma bora na za gharama nafuu kwa wananchi.
Akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari Jijini Dar Es Salaam, leo tarehe 22/02/2022, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari amewaambia wahariri kwamba TCRA imekuwa ikitekeleza jukumu la kuweka mazingira rafiki katika ushindani wa utoaji huduma za mawasiliano kwa kuhakikisha watoa huduma wanajenga ushindani wenye afya ili kuboresha utoaji huduma bora na nafuu kwa wananchi.
Dkt. Jabiri amesema, Serikali kupitia TCRA, imewekeza na kujenga miundombinu yenye gharama kubwa iliyosaidia upatikanaji wa huduma za mawasiliano zilizo bora kwa gharama nafuu hapa nchini ukilinganisha na nchi nyingine Barani Afrika na Ulimwenguni, na kusisitiza kuwa tafiti mbalimbali zimebainisha.
Mathalani bei ya data kwa wastani wa 1GB ni Dola za Kimarekani (USD) 0.750 sawa na shilingi za Kitanzania TZS 1,725. Imeelezwa kuwa mlinganisho wa bei za data mwaka 2021 unaonesha kuwa Tanzania ni nchi ya 6 miongoni mwa nchi 52 barani Afrika, ambazo kiwango cha bei ya data kipo chini kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya utafiti iitwayo British Technology Research Firm.
Kama ilivyo elezwa awali, Barani Afrika Tanzania imo miongoni mwa nchi Kumi kinara kwa unafuu wa gharama ya data inayotumika kwenye simu; hatua hii ni muhimu ikizingatiwa kuwa Serikali imekuwa ikiweka mazingira wezeshi ya uwepo wa watoa huduma wengi wa mawasiliano ya simu ili kuhanikiza ushindani wenye manufaa kwa wawekezaji na kuwapatia wananchi unafuu wa gharama za mawasiliano unaotokana na mazingira ya ushindani kibiashara.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari (wa kwanza kulia) akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wahariri wa vyombo vya habari katika mkutano wa kuangalia mafanikio ya utoaji huduma za data nchini.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.