MRADI wa kitega uchumi wa Jiji la Dodoma unaojengwa ndani ya Mji wa Serikali uliopo Kata ya Mtumba jijini humo umefikia asilimia 78 ya ujenzi ambapo katika awamu ya kwanza unahusisha ukumbi mkubwa wa mikutano, hoteli ya kulala wageni, mabenki, na migahawa.
Hayo yamesemwa na mhandisi anayesimamia mradi huo unaojengwa na Kampuni ya Mohamedi Builders Rayson Merinyo alipokuwa akitoa maelezo ya maendeleo ya mradi huo wakati wa ziara ya madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Songea waliotembelea Jiji la Dodoma kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo uanzishaji na uendeshaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, aliongezea kuksema kuwa gharama za mradi huo kwa awamu ya kwanza ya ujenzi ni shilingi bilioni 18.
Madiwani hao walitembelea mradi huo Septemba 15 mwaka huu ambapo Mhandisi Maronya alisema mradi huo utakapokamilika utakuwa ni chanzo cha kudumu cha mapato kwa jiji hilo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.