MAMLAKA ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetakiwa kuhakikisha inakamilisha hatua za kuwezesha kuanza ujenzi wa vyuo 63 vya Wilaya na kimoja cha Mkoa ili uanze ifikapo Januari 2023.
Hayo yameelezwa hivi karibuni Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda katika kikao cha pamoja kati ya Uongozi wa Wizara na Menejimenti ya VETA.
Kikao hicho kililenga kupokea taarifa ya hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi huo na kuweka mkakati wa utekelezaji wake.
Waziri Mkenda amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma ya elimu ya Ufundi inasogezwa karibu na wananchi hivyo kuhakikisha kila Wilaya ina chuo hicho na kutaka VETA kuhakikisha kazi hiyo ya ujenzi inaanza mara moja na kwa kuzingatia taratibu na sheria husika ikiwemo ya manunuzi.
Mkenda amesema amefarijika na taarifa kuwa tayari Tangazo la 'pre- qualification' limetolewa katika Mfumo wa Kieletroniki wa Manunuzi ya Umma (TANePS) na kutoa rai kwa wakandarasi wenye sifa kujitokeza kushiriki katika fursa hiyo.
"Nimefurahi kuwa sasa kazi imeanza kwa kutoa tangazo la pre- qualification, nawapongeza na naomba kasi iendelee na mhakikishe mnashirikisha wataalamu kutoka taasisi zetu nyingine katika kutoa ushauri ili kazi hii ikamilike katika ubora," amesema Mkenda.
Mkenda ameongeza kuwa Serikali haitavumilia ucheleweshaji wa kazi hiyo kwani ni moja ya eneo la kimkakati katika Serikali na Wizara katika kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanapata ujuzi.
Serikali katika mwaka huu wa fedha imetenga fedha kwa ajili ya kujenga vyuo vya VETA katika Wilaya 63 ambazo hazina vyuo vya Wilaya na kimoja cha Mkoa katika Mkoa wa Songwe.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa VETA, Anthony Kisore ametaja baadhi ya Wilaya zinazojengwa vyuo hivyo kuwa Arumeru, Chamwino, Kondoa, Mpwapwa, Kakonko, Kibondo, Hai, Same, Rorya, Serengeti, Gairo, Bunda, Tarime na Kahama
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.