Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, amesoma hotuba ya mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali, pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021.
"Tangu mwaka 2015 hadi sasa, Serikali imeokoa Sh. bil 19.83 ya mishahara kwa kuwaondoa watumishi hewa 19,708 na vyeti ya kughushi 15,411"
"Hali ya uchumi imeendelea kuimarika, Januari hadi Septemba 2019 ukuaji halisi wa pato la Taifa ulifikia asilimia 6.9 hii ikichangiwa na shughuli za ujenzi kwa asilimia 14.8, madini na mawe 12.6%, habari na mawasiliano 11%, uchukuzi na uhifadhi wa mizigo 88%, na huduma za usambazaji maji 8.5%".
Akiongelea suala la virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa mafua makali (Covid-19), Waziri Mkuu amesema kuwa Tangu kugundulika kwa homa kali ya mapafu (Corona) hapa nchini Serikali inafanya juhudi mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa huu, ikiwemo kuimarisha ukaguzi, upimaji na ufuatiliaji wa wasafiri wanaoingia nchini pamoja na kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaothibitishwa kuwa na ugonjwa huo katika sehemu zilizoainishwa pote nchini.
"Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na uboreshaji wa huduma za jamii nchini kwenye awamu ya tano umezalisha jumla ya ajira mil 12.6"
Ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), ufufuaji wa Shirika la Ndege Tanzania, ufufuaji wa Shirika la mali za Ushirika, ujenzi wa bwawa la ufuaji umeme la Julius Nyerere, uboreshaji miundombinu ya maji, elimu na afya ni kati ya hatua za msingi katika kuhakikisha Tanzania inafika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, amesema Waziri Mkuu.
Aidha, ameongeza kuwa ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka wastani wa TZS Bil. 850 kwa mwezi mwaka 2015 hadi kufikia wastani wa TZS Trilioni 1.3 mwaka 2019, hii ni kutokana na Serikali kuimarisha matumizi ya mifumo ya mapato kwa njia ya kielektroniki.
Changamoto ya maji imetatuliwa kwa kutekeleza ujenzi na ukarabati wa miradi ya maji 1,423, kati ya hiyo 772 imekamilika ambapo miradi 710 ipo vijijini na miradi 82 ipo mijini.
Vilevile, Serikali imeongeza mikopo katika elimu ya juu kutoka TZS Bil. 365 mwaka 2015 hadi kufikia TZS Bil. 450 mwaka 2019 ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu. Pia amesema kuwa Serikali imegharamia ujenzi wa Zahanati 1,198, ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya vipya 487, hospitali za halmashauri za wilaya 69, na hospitali za mikoa 10.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.