Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE
HALI ya ulinzi na usalama katika Mtaa wa Mazengo ni shwari na wananchi wanaendelea kutekeleza shughuli za maendeleo.
Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mazengo, Godfrey Nkinda alipowasilosha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Mazengo.
Nkinda alisema kuwa hali ya ulinzi na usalama katika Mtaa wa Mazengo uliyopo Kata ya Chang’ombe ni shwari. “Uongozi wa serikali ya Mtaa wa Mazengo umekuwa ukishirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha mtaa unakuwa salama. Polisi wamekuwa wakikabiliana na matukio madogomadogo ambayo ni viashiria vya uhalifu. Jeshi la Polisi kupitia Polisi kata na jamii wamekuwa wakifanya doria na misako ili kubaini maeneo chochezi ambayo ni vijiwe vya kuvutia bangi hasa maeneo ya Mapagale jambo ambalo Polisi wamefanikiwa kulipunguza na kazi ya kukabiliana na hali hiyo bado inaendelea” alisema Nkinda.
Alisema kuwa vikao vya ulinzi na usalama vimekuwa vikifanyika kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mtaa kwa kushirikiana na wenyeviti wa mashina ili kuendelea kupeana taarifa juu ya uwepo wa viashiria vya uhalifu.
Kwa upande wake mwananchi wa mtaa huo John Vene alisema kuwa suala la ulinzi na usalama nilawahusu wananchi moja kwa moja. “Hatuwezi kuwategemea Polisi kwa sababu wapo wachache pamoja na kuwa na mafunzo ya kukabiliana na uhalifu” alisema Vene.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.