Serikali imeziagiza Halmashauri 31 ambazo ofisi zao zipo nje ya maeneo yao ya utawala kuhamisha ofisi na kwenda kwenye maeneo yao ya utawala ndani ya siku 30 kuanzia tarehe 07 Oktoba, 2019.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo tarehe 07 Oktoba, 2019 wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na wanahabari mjini Sumbawanga baada ya kupokea maelekezo ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alibaini kuwa halmashauri nyingi hazifanyi kazi katika maeneo yao ya utawala na hivyo kupelekea utoaji wa huduma kusua sua kwa wananchi na kurudisha nyuma maendeleo na mipango ya Serikali.
Waziri Jafo amezitaja halmashauri hizo kuwa ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya Arusha, Halmashauri ya Wilaya Kondoa, Halmashauri ya Wilaya Geita, Halmashauri ya Wilaya Iringa, Halmashauri ya Wilaya Mufindi, Halmashauri ya Wilaya Bukoba, Halmashauri ya Wilaya Mpanda, Halmashauri ya Wilaya Kasulu, Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Halmashauri ya Wilaya Moshi, Halmashauri ya Wilaya Lindi, Halmashauri ya Wilaya Babati, Halmashauri ya Wilaya Mbulu, Halmashauri ya Wilaya Musoma, Halmashauri ya Wilaya Bunda na Halmashauri ya Wilaya Tarime.
Halmashauri nyingine ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya Mbeya, Halmashauri ya Wilaya Kilombero, Halmashauri ya Wilaya Mtwara, Halmashauri ya Wilaya Masasi, Halmashauri ya Wilaya Newala, Halmashauri ya Wilaya Njombe, Halmashauri ya Wilaya Kibaha, Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya Mbinga, Halmashauri ya Wilaya Shinyanga, Halmashauri ya Wilaya Bariadi, Halmashauri ya Wilaya Singida, Halmashauri ya Wilaya Nzega, Halmashauri ya Wilaya Korogwe na Halmashauri ya Wilaya Handeni.
Awali Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alitoa mwezi mmoja kwa watendaji wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kuhamia kwenye Mji mdogo wa Laela ambao umejenga makao yake makuu katika Manispaa ya Sumbawanga wakati lengo la kuanzisha Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga lilikuwa ni kusogeza huduma kwa wananchi lakini mpaka sasa hawajahamisha ofisi zao kwenda katika eneo lao la utawala ambalo ni Mji mdogo wa Laela
Mhe. Magufuli alisema Mkurugenzi wa Halmashauri anatembea kilomita takribani 95 kwenda na kurudi ili awahudumie wananchi wakati kama angekuwepo karibu na wananchi adha zote wanazopata wananchi huduma kufuata huduma zisingekuwepo.
Chanzo: Tovuti ya tamisemi.go.tz
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.